25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAVUNDE ATAKA JWTZ WAPEWE MIRADI YA MAENDELEO

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde, amesema kuna haja Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kutekeleza miradi mbalimbali ya Serikali.

Mavunde alitoa ushauri huo jana, wakati alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa nyumba za walimu na vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi Nzasa,  Manispaa ya Dodoma.

Mavunde, ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini kupitia CCM, alishiriki kwa vitendo ujenzi huo kwa kubeba zege.

“JWTZ wanastahili kupewa ujenzi wa miradi mbalimbali hapa nchini, kutokana na kujenga kwa kiwango kinachotakiwa pamoja na kuonyesha thamani halisi ya fedha.

“Sisi tumeona kazi wanayoifanya, kwanza kazi inakwisha kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa.

“Ujenzi wa nyumba tatu za walimu katika shule hiyo utawasaidia walimu kuishi humo na kuepukana na kero ya kupanga uraiani.

“Kitendo cha walimu kuishi katika mazingira ya shule, kutasaidia kuongeza kiwango cha elimu kwa kuwa watakuwa na muda wa kutosha wa kuwafundisha watoto,” alisema Mavunde.

Naye Msimamizi wa Mradi huo kutoka JWTZ, Kambi ya Ihumwa, Kapteni Ahmed Ligalwike, alisema walipokea Sh milioni 205.5 za mradi huo na kutengeneza madawati 30.

“Kutokana na uwepo wa fedha hizo, JWTZ tuliamua kujenga vyumba viwili vya madarasa na tutaongeza chumba kimoja cha ziada kwa fedha hiyo hiyo.

“Kwa ujumla ni kwamba, fedha hizo zilitengwa kujenga vyoo vitano, lakini sisi tutajenga vyoo saba. Lakini pia, katika bajeti hiyo, hapakuwa na gharama za kuweka miundombinu ya maji, lakini JWTZ tumefanikiwa kuweka miundombinu hiyo baada ya kuona fedha zinaweza kutosha,” alisema Kapteni Ligalwike.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles