MAVUNDE AIPONGEZA KAMPUNI YA MAFUTA PUMA

0
1521

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Antony Mavunde, ameipongeza Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, kwa kuunga mkono juhudi za serikali kwa kujali usalama wa wanafunzi kwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo ya uchoraji kwa wanafunzi wa shule za msingi za mkoa huo.
Amesema tangu mwaka 2013, kampuni hiyo ilipoanzisha kampeni ya usalama barabarani ambayo imekuwa na lengo la kupunguza ajali za usalama barabani na sasa mafanikio yanaonekana.

“Tangu ilipozinduliwa kampeni hii tunaona kuna mafanikio na katika awamu ya kwanza ya mafunzo haya wanafunzi 9,152, wamepewa mafunzo usalama barabarani ikiwamo kushiriki katika michoro hongereni sana Puma.
“….na la kufurahisha zaidi ni hatua ya kuzishirikisha na shule za wanafunzi wenye ulemavu ikiwamo ya shule mojawapo ya Mkoani Ruvuma,” amesema Mavunde.

Awali Meneja Mkuu wa Puma Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema mafunzo hayo ni mwendelezo wa kuwaelimisha wanafunzi kuhusu usalama barabarani tangu mwaka 2013 ilipozinduliwa kampeni hiyo.

“Tangu ilipoanza kampeni hii tumetoa mafunzo kwa wanafunzi wapatao 68,000 katika shule 63 za mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Geita, Kilimanjaro na Ruvuma,” amesema
Alisema madhumuni ya kuwahusisha wanafunzi wa shule za msingi imetokana na kuamini kwamba mafunzo ya salama barabarani yanatakiwa kutolewa kwa watto wadogo ili waweze kukua wakiwa na uelewa kuhusu usalama barabarani.

“Tumeamua kuweka mkazo katika mafunzo haya kwa wanafunzi tukielewa kuwa wanakabiliwa na hatari nyingi za barabarani.

Na kuyafanya mafunzo haya kuwa kipaumbele chetu cha kwanza,” amesema Philippe
Meneja huyo alisema kuwa kwa mwaka huu wamefundisha wanafunzi 9,152 wa shule za msingi 16 za Mkoa wa Dar es Salaam na Ruvuma pamoja na kuendesha mafunzo hayo kwa shule za walemavu na kuwa kampuni ya kwanza ya mafuta kuendesha mafunzo hayo.

Katika mashindano hayo mshindi wa kwanza aliibuka mwanafunzi Francisco Salvatory wa Shule ya Msingi Upanga ambaye alinyakua kitita cha Sh 500,000 wa pili ni Magreth Andrew wa Shule ya Msingi Maktaba, ambaye alivyakua kitita cha Sh 300,000 na wa tatu ni pia alikuwa mwanafunzi wa shule ya Msingi Upanga ambaye alizwadiwa Sh 150,000.
Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here