31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Mavugo aitosa Simba, atimkia Ufaransa

Laudit Mavugo
Laudit Mavugo

Na ADAM MKWEPU -DAR ES SALAAM

NDOTO za klabu ya soka ya Simba za kunasa saini ya mshambuliaji wa Vital’O ya Burundi, Laudit Mavugo, zimeyeyuka  baada ya nyota huyo kutimkia nchini Ufaransa kufanya majaribio katika timu ya Tours FC.

Tangu msimu uliopita Simba ilikuwa ikimsaka Mavugo kwa udi na uvumba, ambapo inadaiwa walimlipa straika huyo sehemu ya fedha za usajili wake kulazimika kusubiri amalize mkataba wake wa mwaka mmoja kuichezea Vital’O.

Kwa mujibu wa Rais wa klabu ya Vital’O, Benjamin Bikorimana, mshambuliaji huyo alisafiri juzi kuelekea nchini Ufaransa kuanza majaribio na klabu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini humo.

“Ni kweli Mavugo yupo nchini Ufaransa,” alieleza Bikorimana bila kutoa maelezo ya kina juu ya safari hiyo.

Akiizungumzia Simba, Bikorimana alisema kwamba bado wanaidai klabu hiyo ya Msimbazi fedha nyingi zikiwemo za usajili wa Amissi Tambwe nayekipiga Yanga kwa sasa.

“Tunaidai klabu ya Simba fedha nyingi kwani hadi sasa hawajamaliza kutulipa fedha za usajili wa Tambwe,” alieleza Bikorimana.

Katika misimu miwili iliyopita, Mavugo aliifungia timu yake ya Vital’O jumla ya mabao 60 na kuiwezesha kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya nchini Burundi kwa mara ya pili mfululizo.

Kabla ya kutua Vital’O, Mavugo aliwahi kucheza katika timu za AS Kigali, Kiyovu na Police FC ambazo zote zinashiriki Ligi Kuu ya Burundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles