Mavitu ya Morrison yamkuna Ngassa

0
626

Winfrida Mtoi, Dar es salaam

WINGA wa Yanga, Mrisho Ngassa, amekunnwa na vya mchezaji mwezake wa timu hiyo, Benard Morrison na kumwagia sifa kutokana na uwezo wake wa kuchezea mpira.

Morrison raia wa Ghana, aliyesajiliwa na Yanga  kipindi cha dirisha dogo lililofungwa  Januari hii, amekuwa gumzo nchini kwa umahiri wake na madoido  ya kuchezea mpira uwanjani.

Mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza winga na mshambuliaji wa kati, katika mechi mbili alizocheza uwanjani zimetosha kumpa umaarufu mkubwa video zake zikisambaa kila kona.

Morrison alianza kuonekana katika mchezo na Singida United, Yanga iliposhinda 3-1, aliwashangaza wapenzi wa soka pale alioochezea mpira kwa mitindo unaojulikana kama kibaiskeli kwenye Uwanja wa Liti, Singida.

Hakuishia hapo, juzi tena alionesha manjonjo hayo dhidi Tanzania Prisons Wanajangwani hao walipoibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kitendo hicho kimemfanya Ngassa ambaye pia ni mtaalam wa kufanya madoido uwanjani, ashindwe kujizua na kuonyesha hisia zake jinsi alivyovutiwa na shoo hiyo.

Ngassa aliandika maneno ya kumsifia nyota huyo katika ukurasa wake wa instagram, vitu hivyo kuna mchezaji angevifanya basi wangemkuta amelazwa hospitali.

 “Hii kitu kuna swahiba wangu mmoja akipiga, mtamkuta hospitali, ‘enjoy soccer,’” aliandika Ngassa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here