27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Maveterani wa kitaa wachuana ndani ya Meridianbet bonanza

Umri Ni Namba Tu, Uwezo Unaonekana!

Ilikua ni wikiendi bomba kwa wanafamilia ya Meridianbet ambao, waliandaa bonaza kabambe la kuwakutanisha maveterani wa mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Lengo kuu likiwa ni kuendelea kudumisha utamaduni wa kufanya mazoezi kupitia michezo mbalimbali, soka ukiwa ni mchezo unaopendwa na sehemu kubwa ya jamii zetu.

Bonanza la mwezi Aprili lililenga kuwakutanisha maveterani wa kitaa ambao, timu zao zilipendekezwa kwa wingi zishiriki tukio hili ambalo lilitangazwa hadharani kupitia mitandao ya kijamii ya Meridianbet. Timu 4 zilizopendekezwa kwa wingi, zilipata nafasi ya kushiriki mtanange huu ambao ulichezwa ndani ya Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza uliwakutanisha Majohe Veterans vs Fire FC ambapo, mchezo ulimalizika kwa ushindi wa magoli 2-0 kwa Fire FC. Mtanange wa pili ulikua kati ya Meridianbet FC vs Kilongawima Veterans, mchezo huu ulitawaliwa na matukio ya piga ni kupige ambazo, magolikipa walikua na kazi za ziada kuzilinda nyavu zao ambazo zilimaliza mchezo bila kutikiswa. Mikwaju ya penati ikatumika kumsaka mshindi na ndipo, Meridianbet FC walipoibuka kidedea kwa penati 5-4.

Mchezo wa kumsaka mshindi wa 3 uliwakutanisha Majohe vs Kilongawima na maveterani wa Majohe kuibuka kidedea kabla ya mchezo wa kumsaka bingwa wa bonanza kati ya Fire FC vs Meridianbet FC kuzichakaza nyavu.

Kwa mara nyingine, mikwaju ya penati iliamua bingwa kati ya Fire vs Meridianbet ambapo, Fire waliibuka kidedea kwa penati 6-5. Hakika, wikiendi ilifana kwa burudani iliyotelewa na timu hizi ambazo zilikua na mashabiki wao uwanjani.

Kama ilivyokawaida ya Meridianbet, washindi walizawadiwa jezi na mipira ikawe sehemu ya kuendeleza juhudi zao za kimichezo na kuimarisha afya zao. Pia, huu ni muendelezo wa Meridianbet kuishirikisha jamii katika masuala mbalimbali yanayoigusa jamii moja kwa moja.Hakika, Meridianbet Ni Familia Kubwa!!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles