23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Mavazi yamzuia Mariah Carey asisafiri

 Mariah Carey
Mariah Carey

LAS VEGAS, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Mariah Carey, amezuiliwa kusafiri katika kiwanja cha ndege, Las Vegas, kutokana na mavazi aliyovaa kuonyesha baadhi ya viongo vyake vya siri.

Inadaiwa kwamba, si mara yake ya kwanza kwa msanii huyo kuzuiwa kusafiri, wiki iliyopita alisimamishwa kwenye uwanja wa ndege mjini Miami kutokana na aina ya nguo alizovaa.

Taarifa zinasema kwamba, msanii huyo alivaa nguo zinazoonyesha sehemu kubwa ya mwili wake eneo la kifua kuonekana jambo ambalo lilisababisha waliomtazama kukasirishwa na nguo hizo.

Hata hivyo, kupitia akuanti yake ya Instagram, aliandika kwamba hakuona sababu ya kuzuiliwa, kwa kuwa mavazi aliyovaa hata watu wengine wanavaa na kusafiri.

“Si mimi pekee nimevaa nguo hizo na kusafiri, wengi wanavaa na kusafiri lakini nashangaa kuona jambo hilo limenikuta mimi, bado mipango yangu ipo pale pale juu ya safari,” aliandika Mariah.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles