25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mauzo soko la hisa yapanda tena

Mary Kinabo
Mary Kinabo

Na JOHANES RESPICHIUS, DAR ES SALAAM

MAUZO katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) imeongezeka kwa asilimia 65 kutoka Sh bilioni 19.6  wiki iliyopita hadi Sh bilioni 32.5 wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Ofisa Mwandamizi wa Masoko wa DSE, Mary Kinabo, alisema kuongezeka huko kumechangiwa na kupanda zaidi ya mara nne kwa hisa zilizonunuliwa na kuuzwa kutoka milioni 2.4 hadi kufikia milioni 9.

Alisema kampuni iliyoongoza kwa hisa zilizonunuliwa na kuuzwa wiki hii ni Benki ya CRDB kwa asilimia 70, ikifuatiwa na Kampuni ya TCC kwa asilimia 25 na Kampuni ya bia TBL kwa asilimia 3.

“Ukubwa wa mtaji wa soko umeshuka kwa asilimia 0.41 kutoka trilioni 21.579 hadi trilioni 21.49, ukiwa umechangiwa na kushuka kwa bei kwenye kaunta za NMG na ACA wakati mtaji wa makampuni ya ndani umepanda kwa asilimia 0.35 kutoka trilioni 8.1 hadi shilingi trilioni 8.13, umechangiwa na kushuka kwa bei kwenye kaunta za TBL,” alisema Mary.

Alisema kiashiria cha sekta ya viwanda wiki hii imepanda kwa pointi 26.16 baada ya bei za hisa za TBL kupanda kwa asilimia 0.77 na sekta ya huduma za kibenki na kifedha imeshuka pointi 0.52 kutokana na kushuka kwa bei kwenye kaunta za DSE kwa asilimia 1.54.

Alisema sekta ya huduma za kibiashara wiki hii imeshuka pointi 4.19 baada ya bei kushuka kwenye kaunta za Swissport kwa asilimia 0.12

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles