24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

MAUWASA yakamilisha mradi wa usambazaji maji mjini Maswa

Na Samwel Mwanga, Maswa

MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa(Mauwasa)iliyoko wilayani Maswa mkoani Simiyu imetumia kiasi cha Sh 509,884,320 ili kukamilisha mradi wa usambazaji wa maji katika mji huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa, Mhandisi Nandi Mathias(kulia) akimtwisha ndoo ya maji Nkamba Sita mkazi wa kijiji cha Iyogelo Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mauwasa, Mhandisi Nandi Mathias amewaeleza Waandishi wa Habari waliotembelea mji wa Maswa kuona utekelezaji wa mradi huo ambao kwa sasa umekamilika na wananchi wameshaanza kupata huduma ya maji safi na salama.

Amesema kuwa mradi huo unajulikana  kama Uboreshaji Huduma ya Maji Maswa Mjini kwa Ustawi wa Taifa kwa Maendeleo katika kupambana na Maambukizi ya Uviko-19.

“Fedha za kutekeleza mradi huu zinatokana na fedha za Uviko 19 ambazo tulizipata kutoka Wizara ya Maji ikiwa ni sehemu ya fedha ambazo Rais Samia Suluhu alipewa kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa huo,”amesema Mhandisi Mathias. 

Amesema  kazi zilizofanyika   kwenye mradi huo ni pamoja na Uchimbaji wa mtaro na kulaza bomba na kufikia urefu wa Kilomita 21.65, ujenzi wa Vituo vinne vya kuchotea maji na ujenzi wa chemba 10.

Mhandisi Mathias amesema hadi sasa mradi huo umekamika  Machi 30,mwaka huu na umeongeza wigo wa Mamlaka hiyo kusambaza maji kutoka asilimia 70 hadi asilimia 80 sambamba na kupata wateja wapya 1000 na kunufaisha mitaa 10  ya mjini Maswa na vijij vitatu.

Ameitaja mitaa hiyo ni pamoja na Mitimirefu, Majengo, SolaMwabomba, Sola, Unyanyembe, Uzunguni, Ujenzi, Jashimba, Ikungulyasubi, Majebele na Badabada.

Vijiji ambavyo vimenufaika naradi huo ni pamoja na  Iyogelo, Buyubi na Matalambuli.

Baadhi ya wananchi wa vijiji vya Iyogelo, Matalambuli na Buyubi waliipongeza serikali kwa kuwafikishia maji safi na salama kwenye maeneo yao.

“Tunaishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kutufikishia maji katika eneo letu kwani tangu tupate uhuru hatujawahi kuwa na maji safi na salama hivyo ni jambo la kuishukuru serikali,”amesema Eva Senga mkazi wa kijiji cha Iyogelo.

Naye Grace Khija mkazi wa kijiji cha Buyubi amesema kuwa siku za nyuma kabla ya mradi huo kuanza kutoa maji walikuwa wakitumia muda mrefu kutafuta maji ambayo walikuwa wakiyapata kwenye mapango ya milima iliyoko kilomita nane kutoka kwenye kijiji hicho na wakati mwingine hupambana na wanyama wakali wakiwemo fisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles