26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

MAUMIVU YA MISULI YAWAKWEPESHA SEREBA WILLIAMS, MARIA SHARAPOVA KUKUTANA

ILE mechi ya tennis iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wapenzi wa mchezo huo kati ya bingwa wa tenisi na raia wa Marekani, Serena Williams na mpinzani wake mkubwa kwenye mchezo huo raia wa Urusi, Maria Sharapova haitochezwa kutokana na Serena kupata maumivu ya misuli.

Muda mfupi kabla ya mechi hiyo iliyokuwa ipigwe leo na mshindi kwenda hatua ya robo fainali mbele ya waandishi wa habari Serena alisema kwamba mara kadhaa amekuwa akihisi maumivu na anatarajiwa kukutana na wataalamu bingwa ili kutambua kiasi cha maumivu yake.

“Kesho nitafanyiwa kipimo cha ‘MRI scan, ntasubiri hadi nikutane na madaktari na pia nitaangalia uwezekano kadri niwezavyo ili niwapate madaktari bingwa. Nitasubiri hadi nipate majibu, nitambue maumivu yangu ni ya kiasi gani.” Alisema Serena mbele ya waandishi wa habari.

Selena alifafanua zaidi kwamba amekuwa akihisi maumivu kwa muda mrefu hivyo anaona mwili wake hauwezi kucheza kwa sasa.

“Kwa bahati mbaya nimekuwa na maumivu kiasi kwenye misuli yangu hivyo ni vigumu kucheza wakati siwezi kutumia vyema mwili wangu.” Alieleza Serena.

Serena anadaiwa kuwa na maumivu hayo tangu alipojifungua mtoto wake Alexis Olympia septemba mwaka jana.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles