23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, March 22, 2023

Contact us: [email protected]

Mauaji kachero wa Serikali gizani

liberatusi-saNA JANETH MUSHI, ARUSHA

SIKU tatu tangu Mkuu wa Idara ya Ulinzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Emily Kisamo, kuuawa kwa kuchinjwa na kichwa kutengenishwa na kiwiliwili, giza bado limetanda juu ya sababu za mauaji hayo.

Mwili wa marehemu Kisamo uliokotwa juzi katika eneo la Kikwarukwaru, Kata ya Lemara jijini hapa ukiwa umefichwa ndani ya gari lake.

Juzi Kamanda Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alipotafutwa kwa njia ya simu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo alisema Desemba 18 mwaka huu Kisamo aliondoka nyumbani kwake saa mbili asubuhi na hakurudi tena mpaka mwili wake ulipookotwa.

Sabas alisema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema wa eneo hilo la Kikwarukwaru kuwa kuna gari limeegeshwa eneo hilo kati ya majira ya saa tatu na nne asubuhi, mpaka saa moja jioni.

Alisema polisi baada ya kupata taarifa hizo, walilazimika kwenda kulichukua gari hilo kwa ‘break down’ na kulipeleka kituo cha polisi.

Alisema baada ya kwenda kulichukua gari hilo lililokuwa limetelekezwa katika eneo hilo, waliliweka kituoni hapo  baadae walipokea taarifa kutoka kwa mke wa marehemu kuwa tangu juzi mumewe aliondoka nyumbani hajarudi na simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

“Wakati tunaendelea na uchugunguzi juzi asubuhi tulilazimika kufungua gari lile na kukuta mwili wa marehemu ukiwa nyuma kwenye buti ya gari huku ukiwa na jeraha nyuma ya shingo”alisema Sabas.

MTANZANIA lilimtafuta Kamanda Sabas jana Jumapili ili kujua upelelezi na juhudi za kuwasaka watuhuniwa hao zilikuwa zimefikia wapi.

Hata hivyo pamoja na kufanikiwa kumpata Kamanda Sabas kwa njia ya simu alidai kwamba alikuwa njiani akiendesha gari na kisha alikata simu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,015FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles