23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

Matumizi ya mishumaa na mafuta ya taa ni hatari- Kotecha

Na Sheila Katikula, Mwanza

Wananchi wa maeneo mbalimbali  ambao hawana umeme katika kata ya Nyamagana jijini Mwanza wameombwa kutumia nishati ya jua ili waweze kupata mwanga na kuacha kutumia taa zinazotumia mafuta ya taa, na mishumaa ili kuepuka majanga ya moto.

Wito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Nyamagana (CCM), Bhiku Kotecha wakati wa uzinduzi wa tawi jipya la ofisi  ya kampuni ya D.LIGHT lililofunguliwa Mkoani hapa.

Alisema ili kuepuka majanga ya moto kila mzazi anawajibu wa kununua taa za nishati ya jua zinazouzwa  na kampuni hiyo ambayo ina mawakala mjini na vijijini kwani lengo lao ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma Salama bila kupata madhara ya kuunguliwa nyumba zao.

Amesema kuna baadhi ya maeneo yanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na  umeme kwa sababu Serikali  bado haijapeleka huduma hiyo ni vema wananchi  kuchangamkia fursa  hiyo ya  kununua nishati hizo.

Hata hivyo amewataka  viongozi hao wa Kampuni hiyo kutembelea kwenye mialo ya Wavuvi ili waweze kutoa elimu ya utumaji wa nishati hiyo  ili  waweze kununua bidhaa hizo na kuepuka  nakutumia kalabai.

Meneja  wa biashara kanda ya ziwa wa kampuni ya D.LIGHT, Saitoti Naikara alisema atahakikisha anazunguka kila sehemu kutoa elimu kwa wavuvi ili waachane na kutumia vifaa ambavyo vinaweza kuwapa hasara katika shughuli zao ambazo zinawaingizia kipato.

Naikara ameongeza kuwa mpaka Sasa wameisha toa ajira kwa vijana ambao ni mawakala zaidi ya 300 kwenye maeneo mbalimbali kanda ya ziwa.

Naye Mtumiaji wa nishati ya jua, Charles Shindika ambae ni mkazi wa Wilaya ya Ilemela amewashauri wananchi kuatumiaji wa bidhaa hizo na kuacha kudanganyika na kutumia mishumaa na taa zinazotumia mafuta ya taa kwani zinaweza kusababisha majanga mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles