25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

MATUMIZI YA INTANETI YANAHITAJI UANGALIFU

NA AZIZA MASOUD,

MAMILIONI ya vijana duniani kote wanatumia intaneti, iwe nyumbani, shuleni, kwenye nyumba za marafiki au kwenye simu zao za mkononi.

Watoto watundu wa sasa wanaielewa sana dunia ya intaneti kuliko wazazi, wapo watoto ambao wanaweza kukuficha mambo wanayoyafanya kwenye intaneti bila wewe kujua.

Ukiwa mzazi au mlezi, kuna mambo ya hatari kuhusu intaneti ambayo yanahitaji uwe mwangalifu zaidi.

Wazazi ambao watoto wao wanatumia intaneti wanahitaji kujua mambo ya msingi kuhusu huduma hiyo na watoto wao wanafanya nini wanapotuma ujumbe mfupi wanapofungua tovuti katika intaneti.

Cha kwanza unapaswa kuangalia sehemu ambayo inatumika kupakulia video ili ujue ni vitu gani vya mtoto huwa anapakua mara kwa mara.

Uchunguzi huo unaweza kuufanya kama mtoto wako anatumia simu yenye uwezo wa intaneti ama kama umemwekea kompyuta ndani itakuwa rahisi zaidi.

Wapo watoto ambao huangalia picha chafu katika  vibanda vya intaneti, hao si rahisi kuwalinda kwa kutumia njia hiyo, badala yake unapaswa kumfanya kutokuwa na mazoea ya kuingia intaneti cafe.

Kundi hilo hutumia muda mwingi kwenye intaneti kwa kuangalia picha za ngono badala ya kuzingatia masomo.

Watu wanaotoa huduma za intaneti na programu za kompyuta wametengeneza programu zinazoweza kuchuja au kuzuia ujumbe unaokuambia ufungue tovuti zisizofaa kwa watoto.

Ni jukumu la kila mzazi au mlezi kuhakikisha watoto wao hawafungui vitu visivyofaa na kuhakikisha wanawapa malezi mema na yenye maadili.

Simu za mikononi na intaneti, licha ya kurahisisha mawasiliano, pia zimekuwa ni kero shuleni, kazini, nyumbani na sehemu nyingine muhimu.

Njia nyingine za kuzuia mtoto asipakue picha za ajabu kwa kuweka kompyuta mahali palipo na uwazi kunawasaidia wazazi kuchunguza kile ambacho watoto wao wanafanya kwenye intaneti na kuweza kuwatia moyo na kuwafundisha wajiepushe na vituo visivyofaa.

Pia mzazi unapaswa kuchunguza jinsi watoto wako wanavyotumia intaneti na uwaeleze kwamba, utakuwa unawachunguza, kufanya hivyo si kuingilia faragha yao.

Uwaweke wazi kwamba dhumuni lako ni kuhakikisha hawaangalii picha mbaya ambazo zitamharibu kimaadili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles