25.3 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Matumizi ya Intaneti yameongezeka nchini-TCRA

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MENEJA Uhusiano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakyanjala, amesema matumizi ya intaneti Tanzania yameongezeka kwa asilimia 4.2 kutoka 29,858,759,204 kwa mwaka 2021 hadi kufikia 31,122,163 kufikia Septemba mwaka huu.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Klabu ya waandishi Mkoa wa Dar as Salaam, (DCPC), Mwakyanjala amesema ongezeko hilo linatokana na mifumo mizuri yenye gharama nafuu iliyowekwa na Serikali.

“Wananchi wanaotumia huduma hii ni wengi hapa nchini sio wa mijini tu bali hata wale wanaoishi vijijini utakuta ana simu yenye uwezo wa kutumia Intaneti,” anasema Mwakyanjala.

Meneja wa Mfuko wa PSSSF, Rajabu Kinande (kushoto), akizungumza na Wanahabari.

Kwa upande wake Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Nchini (UTPC), Deogratias Nsokolo, amewataka waandishi kuacha kuandika habari za kusifia viongozi kwani hazina manufaa kwa wananchi.

“Tunahitaji watu wafichue changamoto zinazowakabili wananchi kwani waandishi wamekuwa wakiandika habari za kusifia sifia watawala badala ya kuandika yale yanayowagusa watu”, anasema Nsokolo.

Katika hali hiyo, Nsokolo ametolea mfano Mkoa wa Kigoma kwamba hakuna meli kwa muda mrefu katika Ziwa Tanganyika.

Kwa upande wake Mwenyeiti wa DCPC Samson Kamalamo, amesema klabu hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa vifaa vya ofisi, hivyo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia ili kuboresha ofisi yao.

Baadhi ya wanachama wa DCPC wakiwa kwenye mkutano ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Rajabu Kinande, amewataka wanachama wanaokaribia kustaafu waanze kushughulikia mafao yao miezi sita kabla ya muda rasmi wa kustaafu ili waweze kulipwa mapema pindi wanapistaafu rasmi.

“Kibali cha kustaafu mfanyakazi anapata miezi sita kabla ya kustaafu, hivyo tunawaomba kushughulikia nyaraka zao ili kuondoa uchelewaji wa kupata mafao yao kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,718FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles