24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Matumaini mgonjwa wa tatu akipona corona

*Mwingine kwa siku tisa mfululizo aonyesha hana maambukizi tena

AVELINE  KITOMARY, DAR ES SALAAM

IDADI ya wanaopona virusi vya corona nchini imeongezeka na kufikia watatu jana huku mgonjwa wa nne naye akiwa na matumaini hayo.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alitangaza jana kupona kwa mgonjwa huyo  wa tatu aliyekuwa na ugonjwa wa homa kali ya Mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (Covid-19)  .

Akitoa taarifa hiyo Waziri Ummy alisema mgonjwa aliyepona alikuwa akiendelea na matibabu katika kituo cha Matibabu Wilaya ya  Ngara, Mkoani Kagera na kufanya Mkoa huo  kutokuwa na mgonjwa  kwa sasa.

“Mungu ni mwema  na leo(jana)  hatuna kesi mpya za Covid-19 ,kupona kwa mgonjwa huyo wa tatu ambaye ni mwanaume,  mwenye historia ya kutembelea kikazi Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC)  na Burundi  kabla ya kukutwa na maambukizi  aliporejea nchini kumeifanya Tanzania kubaki na wagonjwa 16  wa Covid-19  waliopo Dar es Salaam, Arusha na Zanzibar wakiendelea na matibabu na hali zao ni nzuri,”alisema.

Waziri Ummy alisema taarifa za vipimo  kutoka maabara Kuu ya Taifa  zinaonyesha kuwa mgonjwa pekee aliyebaki wa mkoani Arusha  kwa siku tisa hadi kufikia jana vipimo vyake vilikuwa vinaonyesha hana maambukizi tena.

“Ikiwa ni siku ya tisa  sasa baada ya kuanza matibabu ya covid-19  mgonjwa huyo anaendelea kuwa chini ya uangalizi  hadi atakapochukuliwa vipimo vingine  siku  ya 14  ya matibabu yake na kuthibitishwa kuwa hana tena maambukizi  ndipo atakapotangazwa kuwa amepona,”alisisitiza.

Pia, Waziri wa Afya aliwashukuru wananchi kwa kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona hususani kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka. 

Aliwataka wananchi waendelee kuepuka mikusanyiko na misongamano isiyo ya lazima ili kukabiliana na maambukizi.

“ Nawaomba kukaa mita moja au zaidi kati ya mtu mmoja na mtu mmoja ili kuweza kuzuia maambukizi zaidi” alisisitiza.

Aidha katika hatua nyingine ,Waziri wa Afya amekabidhi vifaa kinga kwa Jeshi la Polisi na Magereza kwa ajili ya kujikinga wakati wa kutoa huduma kwa  jamii ikiwa ni msaada kutoka Taasisi ya Jack Maa ya nchini China.

Alisema licha ya asilimia 90 ya vifaa kinga kuelekezwa kwa watumishi wa afya katika vituo vya huduma ya afya nchini, kipaumbele cha Serikali ni kuwakinga watumishi wa afya.

 “Juzi tulimsikia Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania, na mimi nataka kutumia fursa hii kueleza kwamba sisi Serikali tutaendelea kuwalinda watumishi wa afya ili wasipate maambukizi wakati wanapotoa huduma kwa wagonjwa,” alisema Ummy Mwalimu.

Amevitaja vifaa kinga vilivyotolewa kwa Jeshi la Polisi na Magereza  ni pamoja na Barakoa 16,000 , gloves 8,000, nguo za kujikinga (PPE) 50 na jiki ya vidonge kopo (chlorine) 100. 

Alisema kuwa wizara yake imetoa vifaa hivyo ikiwa ni msaada kutoka kwa Jack Maa kwa sababu  Jeshi la Polisi na Magereza wamekuwa wakikutana mara kwa mara na wananchi na pia wamekuwa wakisaidia kazi mbalimbali za kuhudumia jamii ikiwemo kutoa huduma za afya kwenye vituo vyao. 

Waziri Ummy alileleza  kuwa vifaa hivyo vitatumika kwa ajili ya vituo vya afya vya Jeshi na kwa ajili yao wenyewe wakati wa kutoa huduma kwa wananchi.   

“Lengo letu ni kuhakikisha pia kwamba vituo vyote vinatoa huduma kwa jamii hususani jeshi la Polisi na Magereza tunawapatia vifaa tiba ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona,” alisema.

Kwa upande wake ,Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Utawala wa Jeshi hilo, Anthon Ruta alishukuru kwa kubabidhiwa vifaa kinga kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa vya Corona na kuvitumia kutokana na maelekezo yaliyotolewa.

Naye Mkaguzi Msaidizi na Ofisa Tabibu wa Jeshi la Magereza, Kenazi William alisema kuwa wanashukuru kwa kupatiwa msaada ambao umekua ni chachu  kwao kwa kuwa wamekuwa wakipokea wageni wengi wakiwamo mahabusu,.

Machi 16 kwa mara ya kwanza Waziri Ummy aliripoti uwepo wa mgonjwa wa virusi vya Corona nchini ambapo hadi sasa idadi ya wagonjwa imefikia 20 huku mgonjwa mmoja akifariki dunia na wengine watatu kupona ugonjwa huo.

Mwishooo…..

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles