24.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Matola afichua siri makali ya Lipuli

MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

KOCHA wa Lipuli FC, Seleman Matola, amefichua siri ya kikosi chake kuendelea kukusanya pointi tatu katika Ligi Kuu Tanzania Bara inayoendelea.Lipuli imefanikiwa kukusanya pointi tisa kupitia michezo yake mitatu mfululizo ambayo ni dhidi ya Mbeya City iliposhinda mabao 2-0 ugenini, ikaizamisha Ruvu Shooting kabla ya kuitungua Biashara United.

Akizungumza na MTANZANIA, Matola alisema sare waliyopata dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, iliwaongezea ujasiri wa kupambana wachezaji wake katika michezo iliyofuata na kufanikiwa kushinda michezo hiyo mitatu mfululizo.

“Kwa sasa Lipuli tupo vizuri baada ya kupata sare na Simba kuna nguvu mpya ambayo imeingia kwa wachezaji, kwa sasa wanajiamini na kutumia uwezo wao wote wakiwa uwanjani hali inayosaidia kuweza kupata matokeo hivyo bado moto hauzimwi kwa sasa.

“Tumejipanga kufanya vizuri katika michezo yetu yote tutakayocheza kwa sasa, hilo linawezekana kwani mpira ni mchezo ambao hauwezi kuficha matokeo yake yanapatikana uwanjani, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” alisema Matola.

Lipuli inakamata nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi 22, baada ya kushuka dimbani mara 17, ikishinda michezo mitano, sare saba na kupoteza michezo mitano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles