28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 19, 2022

Matokeo kidato cha Pili yatangazwa, ufaulu waongezeka

 Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) leo Ijumaa Januari 4, limetangaza matokeo ya mitihani ya Kidato cha Pili illiyofanyika Novemba mwaka jana, ambapo ufaulu umeongezeka kulinganisha na mwaka 2017.

Akisoma matokeo hayo leo Katibu Mkuu wa Baraza hilo Dk. Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 545,077 waliosajiliwa kufanya mitihani hiyo waliofanya ni 506, 235 sawa na asilimia 92.87.

“Wanafunzi 38, 842 sawa na asilimia 7.13 hawakufanya mitihani kutokana sababu mbalimbali zikiwamo utoro na ugonjwa,” amesema Dk Msonde.

Dk Msonde wanafunzi 452,273 sawa na asilimia 89.68 wamepata alama zitakazowawezesha kuendelea kidato cha Tatu na wanafunzi 52, 073 sawa na asilimia 10.32 wamekosa alama zitakazowawezesha kuendelea na kidato cha Tatu.

“Mwaka 2017 wanafunzi 433,453 sawa na aasilimia 89.32 walipata alama za kuwawezesha kuendelea na masomo ya kidato cha Tatu, hivyo ufaulu wa ujumla umeongezeka kwa asilimia 0.36, ” amesema.

Aidha Baraza linatoa wito kwa walimu na na Wanafunzi wahakikishe ufundishaji na kujifunza kunaimarishwa katika masomo yote shueleni ili kuwawezesha wanafunzi kupata umahiri unaostahili katika kuboresha elimu nchini.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,312FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles