24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MATIBABU YA SCHUMACHER YAFIKIA BILIONI 36/-

GENEVA, USWISI


 

BINGWA wa zamani wa mchezo wa Formula One, Michael Schumacher, hadi sasa inaripotiwa kuwa matibabu yake yamefikia kiasi cha pauni milioni 14 zaidi ya Sh bilioni 36 tangu alipopata ajali Desemba 29, 2013.

Nyota huyo wa magari alipata ajali ya gari na kusababisha matatizo ya kichwa ambapo alipoteza fahamu kwa muda mrefu, tangu apate ajali hiyo hadi sasa bado hali yake haijakaa sawa na anaendelea na matibabu huko nyumbani kwake Geneva nchini Uswisi.

Matibabu yake kwa kipindi cha miaka mitatu tangu amepatwa na tatizo hilo kwa sasa yamekuwa juu huku bado hali yake imekuwa ya kusuasua japokuwa imekuwa tofauti na miaka miwili iliyopita.

Inadaiwa kwamba, nyota huyo wa magari matibabu yake kwa wiki yanafikia kiasi cha pauni 115,000, ambapo ni sawa na 303,582,000 kwa wiki, hivyo kuweza kufikia kiasi cha pauni milioni 13.8, sawa na bilioni 36.

Thamani ya nyota huyo wakati yupo katika mashindano miaka mitatu iliyopita ilifikia kiasi cha zaidi ya pauni milioni 500, ambazo ni sawa na zaidi ya Sh bilioni moja.

Mke wa nyota huyo, Corinna Betsch, amedai kuwa anaendelea kupambana ili kuhakikisha hali ya mume wake inaendelea kuwa kama awali.

Corinna alifanya maamuzi ya kuuza ndege ya mume wake kwa ajili ya kutenga fedha za matibabu, lakini hadi sasa bado hali haijatengemaa.

Meneja wa Schumacher, Sabine Kehm, amedai kwa sasa hawana mpango wa kueleza kile ambacho kinaendelea katika hali ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 47.

“Tunaendelea kupambana kuhakikisha Schumacher anarudi katika hali yake ya kawaida, lakini si jambo la msingi kuueleza umma hali jinsi inavyoendelea, tutaendelea kulinda kile ambacho tumekipanga.

“Habari ambazo zitakuwa zinaenea bila kutoka kwa watu husika zitakuwa hazina ukweli wowote, familia itaweka wazi nini kinaendelea kama itahitajika kuwa hivyo,” alisema Kehm.

Meneja huyo aliongeza kwa kuwaomba wadau mbalimbali waendelee kufanya maombi kwa ajili ya nyota huyo aweze kurudi katika hali yake.

“Tunathamini mchango wake, tunatambua yale ambayo ameyafanya katika michuano ya Formula One, hivyo ni vizuri kumwombea aweze kurudi katika hali yake ya kawaida, amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu sasa ni vizuri kumwombea,” aliongeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles