27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

MATERAZZI: SITOSAHAU KICHWA CHA ZIDANE

A photo taken 09 July 2006 shows French

CHENNAI, INDIA

NYOTA wa zamani wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Inter Milan, Marco Materazzi, amedai kuwa hatakuja kumsahau nyota wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Zinedine Zidane, kutokana na kumtwanga kichwa katika fainali za Kombe la Dunia 2006.

Imepita miaka 10 sasa tangu tukio hilo litokee katika fainali hiyo ambapo Zidane alimpiga kichwa nyota huyo baada ya kupishana kauli ndipo Zidane akatolewa nje kwa kadi nyekundu.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Materazzi amewakumbusha mashabiki tukio hilo ambalo amedai kuwa hawezi kulisahau katika maisha yake.

Beki huyo wa zamani aliweka picha ya tukio zima jinsi lilivyokuwa pamoja na tuzo ambazo walizipata baada ya kumalizika kwa fainali hiyo ambayo ilipigwa kwenye Uwanja wa Olympiastadion Berlin nchini Ujerumani.

Baada ya tukio hilo, Zidane aliweka wazi kuwa Materazzi alikuwa anamzungumzia mama wa kocha huyo wa sasa wa klabu ya Real Madrid na ndio maana akachukua uamuzi huo.

Lakini katika picha hiyo ambayo Materazzi aliiweka kwenye akaunti yake ya Instagram, aliweka wazi kuwa hakumtaja mama yake Zidane, ila alikuwa anamzungumzia dada yake.

“Ni kweli jambo ambalo nililiongea lilikuwa la kijinga, lakini sikustahili kufanyiwa vile na Zidane, ukiwa katika mitaa ya mjini Naples, Milan na Paris utasikia maneno makali zaidi ya yale ambayo niliyaongea uwanjani lakini ni jambo la kawaida.

“Ukweli ni kwamba wakati ule mama yake Zidane alikuwa amelazwa hospitali, lakini sikuongea neno lolote ambalo lilikuwa linamhusu mama huyo, ila nilikuwa namzungumzia dada yake.

“Mama yangu alipoteza maisha tangu nikiwa na umri wa miaka 15, hivyo siwezi kumzungumzia mama yeyote kwa kuwa naguswa na mama,” aliandika Materazzi.

Kwa sasa Materazzi ni kocha wa klabu ya Chennaiyin FC ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini India.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles