22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Matarajio bajeti kuu

Na Fredy Azzah

-Dar es Salaam

LEO Serikali inatarajia kusoma Bajeti Kuu ya zaidi ya Sh trilioni 33 kwa mwaka wa fedha 2019/20, kutoka bajeti ya Sh trilioni 32 mwaka 2018/19, huku wananchi na wadau wengine wakieleza matarajio yao.

Machi mwaka huu, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisoma kwa wabunge Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2019/20, akisema Serikali inatarajia kutumia Sh trilioni 33.1.

WIZARA NANE ZASOMBA TRIL. 30/- 

Hadi sasa wizara zote 21 zimeshaidhinishiwa na Bunge fedha zilizoomba kwa matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka wa fedha 2019/20, huku nane pekee zimesomba zaidi ya Sh trilioni 30.

Wizara ambazo zinachukua zaidi ya Sh tirilioni 30 kati ya Sh trilioni 33 zinazotarajiwa kugawanywa kwa wizara zote 21, ni pamoja na Fedha na Mipango ambayo imetengewa Sh trilioni 11.94, ambazo kati yake fedha za maendeleo ni Sh bilioni 730.6.

Nyingine ni Ofisi ya Rais (Tamisemi), iliyotengewa Sh trilioni 6.21, kati yake fedha za fedha za maendeleo Sh trilioni 1.69; Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sh trilioni 4.96, kati yake za maendeleo Sh trilioni 4.8 na Nishati Sh trilioni 2.14, kati yake fedha za maendeleo Sh trilioni 2.11.

Nyingine ni Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Sh trilioni 1.85, kati yake fedha za maendeleo Sh bilioni 128;  Elimu Sayansi na Teknolojia Sh trilioni 1.39, kati yake za maendeleo Sh bilioni 826.7; Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Sh bilioni 690.7, kati yake fedha fedha za maendeleo Sh bilioni 546.9 na Mambo ya Ndani ya Nchi Sh bilioni 921.2, kati yake fedha za maendeleo Sh bilioni 31.

WIZARA 13 ZAGAWANA TRIL. 3/-

Wizara nyingine 13 zitakazogawa Sh trilioni tatu zilizobaki ni pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotengewa Sh bilioni 148.9, kati yake Sh bilioni 62.6 zikiwa za maendeleo, Sh bilioni 124.2 Bunge na Sh bilioni 7.6 maendeleo ya Bunge.

Nyingine ni Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Sh bilioni 683.5, kati yake maendeleo Sh bilioni 199.9;  Ofisi ya Makamu wa Rais Sh bilioni 36.9, kati yake fedha za maendeleo Sh bilioni 19.2; Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Sh bilioni 30.9, kati yake fedha za maendeleo Sh bilioni 9.3 na Maji na Umwagiliaji Sh bilioni 634.2, kati yake fedha za maendeleo Sh bilioni 610.5.

Wizara nyingine ni Viwanda na Biashara Sh bilioni 104, kati yake fedha za maendeleo Sh bilioni 51.5; Kilimo Sh bilioni 253.9, kati yake fedha za maendeleo Sh bilioni 143.6; Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi Sh bilioni 24.9, kati yake za maendeleo Sh bilioni 17.7 na Maliasili na Utalii Sh bilioni 120.2, za maendeleo Sh bilioni 48.8 na.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Sh bilioni 62.7, kati yake za maendeleo Sh bilioni 6.2; Madini Sh bilioni 49.5, kati yake za maendeleo Sh bilioni 12.5;  Sheria na Katiba Sh bilioni 181.3, kati yake za maendeleo Sh bilioni 30.1 na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Sh bilioni 166.9, za maendeleo Sh bilioni 4.

BAJETI 2018/19 ILIVYONG’ATA, KUPULIZA

Bajeti inayoisha pamoja na mambo mengine, Serikali ilisamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye vifungashio vya dawa za binadamu kwa viwanda vinavyozalisha dawa hapa nchini, kusamehe kodi ya ardhi kwa taasisi za Serikali kwa sababu hazitengenezi faida na kufuta na kupunguza baadhi ya viwango vya tozo na ada zinazotozwa sekta ya uzalishaji wa chumvi. 

Pia ilisamehe VAT kwenye taulo za kike, ilipunguza kiwango cha kodi ya mapato ya kampuni kutoka asilimia 30 hadi 20 na kutoa msamaha wa kodi ya zuio inayotozwa katika riba kwa mikopo inayotolewa kwa Serikali na benki, taasisi za fedha na wahisani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Serikali.

Katika bajeti hiyo, Serikali ilifanya mabadiliko ya kiwango cha kodi katika michezo ya kubahatisha ya ubashiri wa matokeo ya michezo (sports betting) kutoka asilimia 6 ya mauzo ghafi hadi asilimia 10. 

Pia iliongeza kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye michezo ya kubahatisha (Casino) kutoka asilimia 15 hadi asilimia 18 ya mapato. Pia kodi ilipanda kwenye vinywaji kama soda, bia na vinywaji vikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles