26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Matapeli wapiga hodi sekta ya kilimo, mifugo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari.

Na Pendo Fundisha, Mbeya

KUNDI la watu wanaohofiwa kuwa ni matapeli, limeibuka mkoani Mbeya na kuwatapeli wananchi kupitia uuzaji na usambazaji wa dawa za mifugo na kilimo.

Watu hao wanaosemekana ni matapeli wa kimataifa, wamekuwa wakitumia njia ya mawasiliano ya simu kuwatapeli wakulima na wafugaji pamoja na wafanyabiashara wa maduka ambao huwadanganya kuwa ni wasambazaji wakubwa wa dawa hizo na kuwashawishi kufanya biashara nao na mwisho wa siku  kuwatapeli.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari, umebaini kwamba matapeli hao wameamua kutumia fursa ya kilimo na ufugaji katika kujipatia kipato kwa njia ambayo si halali.

Matapeli hao wamekuwa wakiwafuatilia baadhi ya wakulima na wafugaji kwa kula njama na majirani au ndugu wa karibu na kufanikiwa kupata mawasiliano na kupiga simu kwa muhusika kwa kujifanya wao ni mawakala na wasambazaji wakubwa wa dawa hizo muhimu kutoka mkoani Arusha na kwamba wanashirikiana na mataifa makubwa ya Ulaya.

“Kazi kubwa wanayoifanya watu hawa ni kuhakikisha wanapata mawasiliano ya mlengwa na kisha kumpigia simu na kumshawishi kufanya biashara naye,” alisema Kamanda Kidavashari.

Alisema ‘wapigaji’ hao wameonekana kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri kwani wanaenda na alama za nyakati, baada ya kuona Watanzania wameamua kuwekeza kwenye mifugo na kilimo, sasa wameingia huko na kuendeleza mchezo wao wa uhalifu.

Alisema kazi kubwa inayofanywa na watu hao ni kuwaeleza wahusika kwamba wanasambaza dawa hizo za mifugo na kilimo na kuwataka wafugaji kutuma fedha kwa kutumia mitandao ya simu ya Tigo pesa, M-Pesa na Airtel Money.

“Matapeli hawa ukizungumza nao watakueleza tuma kiasi cha fedha kwa ajili ya kianzio, lakini wanakueleza unatakiwa kuzituma kwa njia ya simu na si huduma za kibenki, hivyo ukimsikia mtu huyu ni vema ukamuogopa na kutoa taarifa polisi,” alisema.

“Matapeli hawa hawezi kwenda kwa mtu ambaye hana tamaa, huenda kwa mtu ambaye tabia yake hupenda maisha mazuri na kwa njia rahisi  ya kupata fedha haraka,” alisema.

“Mtu anayekuumiza ni jirani yako au ndugu wa karibu kwa kutoa taarifa zako, hivyo watu wanatakiwa kuwa na tahadhari wasiishi kwa mazoea, bali kwa kujihami na kwa hisia zaidi katika maisha ya sasa,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles