28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mata aipa ubingwa Manchester United

during the Barclays Premier League match between Manchester UnitMANCHESTER, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa timu ya Manchester United, Juan Mata, anaamini kuwa klabu hiyo itafanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Mchezaji huyo amesema timu hiyo ilikuwa na wakati mgumu katika baadhi ya michezo yake, lakini kwa sasa ipo katika nafasi nzuri ya kuweza kuchukua ubingwa wa michuano hiyo.

Klabu hiyo inajivunia kucheza michezo minne mpaka sasa bila kufungwa mara baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Arsenal, ambapo walipokea kichapo cha mabao 3-0.

“Ngoja tuone kitakachotokea, maana lengo letu ni kupambana katika kila mchezo ili kujihakikishia tunabeba taji la Ligi Kuu msimu huu.

“Tulikuwa katika kipindi kigumu katika baadhi ya michezo iliyopita, lakini kwa sasa tunaweza kusema tupo katika nafasi mzuri ya kufanya vizuri kutokana na michezo iliyosalia kumaliza mzunguko wa kwanza,” alisema Mata.

United kwa sasa inashika nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi baada ya kucheza michezo 12 na kufanikiwa kupata alama 24, wakati majirani zao, Manchester City wakiongoza huku wakiwa na alama 26.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles