29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 20, 2021

MASTAA WALIOPATA WATOTO WAKIWA NA MIAKA 50

Na MWANDISHI WETU


WATAALAMU wa masuala ya afya wanasema mwanamke akifikisha umri wa miaka 50 anaweza kupata matatizo ya kizazi kama hatapata mtoto hadi umri huo, lakini anaweza kupata ujauzito na akajifungua salama.

Wataalamu hao wanasema kwa mwanamume hata anapokuwa na miaka 60 bado ana uwezo wa kutoa mbegu zenye uwezo wa kutengeneza mtoto, lakini kwa mwanamke kuna asilimia chache za kupata mtoto kwani wakati mwingine hata wakipata ujauzito huharibika kabla ya kujifungua na kama akizaliwa anaweza kupata matatizo ya kiafya, lakini wataalamu hao wanasema pia mwanamke huyo anaweza kupata ujauzito na akajifungua mtoto salama na akaishi bila matatizo.

Wataalamu hao pia wanasema kwa mwanamke kupata mtoto wa kwanza akiwa na miaka 35 anaonekana kama amepata akiwa kwenye umri wa uzee.

Orodha iliyotolewa mwaka 2012, wanawake 154 wenye umri zaidi ya miaka 50 waliopata watoto kwa mara ya kwanza duniani kote, watoto wengi walizaliwa wakiwa na matatizo ya kiafya, mwaka 2000 waliojifungua watoto wa aina hiyo walikuwa 44 na mwaka 2008 walikuwa 69.

Wafuatao ni baadhi ya mastaa waliofanikiwa kupata watoto wakiwa na umri mkubwa na watoto wao wamezaliwa salama.

Janet Jackson

Huyu ni mwanamuziki wa Pop nchini Marekani, dada wa aliyekuwa mfalme wa muziki wa Pop, Michael Jackson (marehemu). Mei 16 mwaka huu atatimiza miaka 51, alifanikiwa kupata mtoto wa kwanza Januari mwaka huu akiwa na miaka 50, aliolewa na mfanyabiashara Wissam Al Mana raia wa nchini Qatar, lakini kwa sasa wameachana.

Janeth aliwahi kufunga ndoa zaidi ya mara moja akiwa na umri wa miaka 18 tu lakini hakufanikiwa kupata mtoto, aliolewa na James DeBarge mwaka 1984 na mwaka mmoja baadaye aliachika akaolewa na Rene Elizondo Jr mwaka 1991 na mwaka 2000 wakaachana.

Carole Hobson

Huyu ni msanii wa zamani wa muziki nchini Uingereza, licha ya kiu yake kubwa ya kupata mtoto alipokuwa na miaka 50, aligundulika kuwa ana matatizo ya kizazi.

Kwa kuwa alitamani sana mtoto wa kumzaa aliamua kutumia pauni 20,000 zaidi ya milioni 55 za Kitanzani kwa ajili ya matibabu ya kusafisha kizazi chake ili aweze kupata mtoto.

Lakini alipotimiza miaka 58 ilikuwa Sikukuu ya Krismasi mwaka 2010, alifanikiwa kupata watoto mapacha na akawa staa wa kwanza nchini Uingereza kupata mtoto akiwa katika umri mkubwa ingawa watoto hao awali walipatwa na matatizo ya kiafya, kwani walipokuwa na miezi miwili kila mmoja alikuwa kwenye uzito wa kilo mbili lakini kwa sasa wanaishi vyema na wana afya njema.

Tina Malone

Huyu ni staa mwingine kutoka nchini Uingereza, alinga’ra zaidi kwenye filamu ya ‘Shameless’.

Mwigizaji huyu mwenye miaka 54 sasa, anadai kwamba mwanzo alishangaa alipomwona rafiki yake wa karibu, Marcia Cross, akipata mtoto akiwa na miaka 44 akaamini naye atapata hata akifika miaka 50.

Imani yake iliendelea hivyo alipofikisha miaka 50 kweli akafanikiwa kupata ujauzito na akajifungua mtoto wake wa kwanza salama.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,594FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles