23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

Mastaa waliofuata vipaji vya wapenzi wao

Diamond Plutnumz
Diamond Plutnumz

NA CHRISTOPHER MSEKENA,

MAPENZI kizunguzungu. Aliimba msanii wa Bongo Fleva, Rachel. Ni kweli mapenzi yanaweza kumfanya mtu asione ingawa ana macho au akawa tayari kubadili jambo fulani kwa ajili ya mpenzi wake.

Ndivyo ilivyo. Mapenzi yana nguvu sana. Katika ulimwengu wa mastaa, wapo baadhi ambao waliamua kwa nyakati tofauti kufanya vitu ambavyo wenzi wao wanavifanya kwa lengo la kutafuta furaha yao au wapenzi wao.

Ili uone kwa ni namna gani mapenzi yalivyo na nguvu,  watazame mastaa ambao kutokana na kuwa na uhusiano na wasanii wa muziki au filamu nao wamejikuta wakitumbukia katika sanaa hizo.

Hapa chini nitakupa listi ya baadhi ya wasanii wa Bongo ambao kwa namna moja ama nyingine walibadilisha upepo na kuingia kwenye fani za wapenzi wao.

Hata hivyo, wapo ambao walitoka kisanii na mpaka sasa wanaendelea kufanya vizuri katika sanaa husika huku wengine wakishindwa kufurukuta.

SHILOLE

Alianza kufahamika kupitia filamu za Kibongo. Anasifika kwa uwezo wake wa kuvaa uhusika na kufanya kazi nzuri anapokuwa mbele ya kamera. Ila alipotua kwenye muziki watu wengi walihoji ina maana filamu hazilipi?

Kama ulikuwa hufahamu, Shilole amewahi kutoka kimapenzi na fundi wa muziki, Elias Barnaba ‘Barnaba Boy’. Inasemekena Barnaba ndiye aliyemuingiza rasmi Shilole kwenye muziki huku akimpa sapoti ya kumuandikia mashairi ya baadhi ya nyimbo zake.

Hakuna ubishi, mafanikio ya Shilole kumuziki yana mchango mkubwa sana wa Barnaba.

SNURA
Snura Mushi

 

SNURA

Ni machachari mno kwenye filamu, alianza kupata umaarufu aliwa kwenye tasnia ya filamu lakini huwezi amini hivi sasa anautikisa muziki wa Bongo Fleva na ngoma yake mpya inayoitwa Shindu.

Snura Mushi alichomoa posa ya Dj Hanter, mkali anayechezesha muziki kwenye klabu ya Maisha, huko Morogoro. Wamekuwa ni wapenzi kwa muda mrefu na Snura ameshawishika kuziweka pembeni filamu na kujikita kwenye muziki sababu ya kuwa karibu na Dj huyo kimapenzi.

Kama ulikuwa hujui, habari ya mjini ndiyo hiyo.

DIAMOND

Crazy Tenant ni filamu iliyoonyesha kipaji kingine cha staa wa muziki Bongo, Diamond Platnumz. Filamu hiyo ilichezwa mwaka 2012 huku mhusika mkuu akiwa ni Peter Msechu na Wema Sepetu. Diamiond alichomoza katika vipande kadhaa.

Mtayarishaji wa filamu hiyo, Selles Mapunda  alisema kabla haijapewa jina hilo la Kizungu, ilitakiwa kuitwa Nimpende Nani na Diamond alitakiwa awe mhusika mkuu.

Mapenzi ya Wema na Diamond yalimfanya staa huyu wa ngoma ya Kidogo kujihusisha na filamu japokuwa yeye ni mkali wa kuimba. Baada ya sinema hiyo, Diamond hajacheza filamu nyingine.

ISABELLA

Huyu ni Miss Ruvuma mwaka 2006 ambaye alikuwa mpenzi wa msanii wa Bongo Fleva Luteni Kalama. Isabella ni msanii wa filamu, lakini kwa kutoka na Kalama aliingia pia kwenye muziki.

Kutoka kimapenzi na Kalama kulichagiza mrembo huyu naye kuanza kujihusisha na masuala ya muziki. Mapenzi yalifanya aziweke kando filamu na shunguli za urembo na kujikita kwenye muziki akiwa na mwenzake Jini Kabula.

Wawili hao wanaunda Kundi la Scorpion Girls.

 

MOSE IYOBO

Kama wewe ni mpenzi wa filamu za Kibongo basi hii inaweza kuwa habari njema kwako. Mkali wa kudansi nchini Mose Iyobo hivi karibuni ameweka wazi mipango yake ya kufanya filamu na mpenzi wake Aunt Ezekiel pamoja na mtoto wao Cookie.

Hii ni filamu ya familia. Mapenzi yana mchango wake katika kumuhamisha Mose Iyobo kutoka kwenye kudansi mpaka filamu.

Je, huko atamudu na kuwafunika mastaa wengine wa kiume? Je, ataweza kufikia kiwango cha mpenzi wake Aunt Ezekiel ambaye kwa sasa ni miongoni mwa mastaa bei mbaya? Tusubiri tuone.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles