24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 23, 2023

Contact us: [email protected]

MASTAA NA PENZI LA BANDIKA BANDUA

Na JOHANES RESPICHIUS

USTAA ni mzigo! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na namna maisha yao yanavyoandamwa na vyombo vya habari.

Hata hivyo, ukitazama upande wa pili utaona kuwa mastaa na vyombo vya habari ni kama samaki na maji. Staa hawezi kuishi bila kuunganishwa na vyombo vya habari.

Maisha ya staa ni habari. Hiyo ndiyo sababu unaweza kushangaa jambo fulani linafanywa na mtu fulani huko uswahilini lakini haliwi habari ila akifanya staa linaripotiwa!

Hakuna namna nyingine, ngoja tuendelee kuandika. Siku za hivi karibuni kumekuwa na tabia ya wasanii kuwa kwenye uhusiano na wenzi waliozidiana umri mkubwa.

Mifano ipo mingi na hata Swaggaz tumewahi kuripoti kapo za mastaa waliozidiana umri. Leo tunakupa kitu kingine kipya. Wapo wasanii ambao wanaingia kwenye uhusiano, kisha baada ya muda uhusiano unavunjika – hilo ni jambo la kawaida.

Lakini stori ni pale ambapo wanapoachana na wenzi wao, muda mfupi baadaye wanaingia kwenye uhusiano mpya – bandika bandua.

Fukunyunyu za Swaggaz kitaani zinaeleza kuwa, mastaa wanaoongoza kwa kufanya hivyo ni wa kike, huku ikidaiwa kuwa hufanya hivyo kwa lengo la kuwaumiza moyo wenzi wao waliowatema.

Huenda listi ni ndefu zaidi, lakini Swaggaz inakuletea kwako mastaa hawa hapa chini.

 

WOLPER, BROWN

Haukupita muda mrefu kwa staa huyu wa Bongo Muvi, Jacquline Wolper kuingia katika uhusiano na kijana ambaye inasemekana ni modo baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Rajabu Abdallah ‘Harmonize’, staa wa Bongo Fleva kutoka Wasafi Classic Baby (WCB).

Hata hivyo inaelezwa kuwa Brown ni mdogo kiumri kuliko Wolper. Hii siyo mara ya kwanza kwa Wolper kuamua kuwa mapenzini na Serengeti Boy kwani hata penzi lake na Mkongomani lilipoisha aliamua kutafuta pumziko kwa Harmonize.

Licha ya mwanzo kupinga kuwa Brown siyo mpenzi wake bali ni rafiki yake wa daima (Best Friend Forever – BFF) lakini ni dhahiri kuwa uhusiano huo ni kwa ajili ya kumuumiza Harmonize.

Mara kwa mara Wolper amekuwa na kawaida ya kumsifia mpenzi wake huyo mpya kwa kuandika maneno matamu katika ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram.

Moja ya maneno aliyowahi kuandika Wolper kupitia Instagram ni kwamba alikutana na Brown miaka minne iliyopita, huku akitaja sababu iliyomfanya avutiwe naye kuwa ni upole na ukweli.

NISHA, MINU

Mwigizaji Salma Jabu ‘Nisha’ naye ishu hii hajamwacha salama. Nisha katika kuwaziba watu midomo juu ya uhusiano wake wa sasa, kwenye akaunti yake ya  Instagram amebadilisha jina na kuwa Nisha Minhal Azad ambapo majina mawili ya mbele ni ya mpenzi wake huyo ambaye anafanya muziki wa Bongo Fleva.

Kabla ya Nisha kuingia katika uhusiano wa kimapenzi na ‘Serengeti Boy’ huyo, alikuwa anatoka na msanii wa Bongo Fleva, Baraka Andrew ‘Barakah The Prince’ hiyo ni baada ya kuachana na staa wa muziki wa Hip Hop, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.

 

SAJENT, DULA MAKABILA

Mrembo Husna Idd maarufu Sajent, yupo mapenzini na mkali wa muziki wa Singeli anayetamba na singo Makabila na Ujauramba, Dulla Makabila.

Sajent alimhakikishia polisi wa Swaggaz kuwa yupo ndani ya penzi jipya kutoka kwa kijana ambaye anamzidi kiumri na kwamba anayafurahia maisha ya sasa kwani amepata mpenzi anayemfanya asijisikie mpweke hivyo hajutii kuwa na Makabila.

Makabila anaziba nafasi ya mkali wa filamu Salim Ahmed ‘Gabo Zigamba’ ambaye anafanya vizuri na sinema yake ya Kisogo na Siya Bonga.

Tangu uhusiano wa Gabo na Sajent uvunjike ni kipindi kifupi tu kabla ya kuamua kuingia kwenye penzi jipya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,093FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles