29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Mastaa hawa Afrika bado wanaweza kuhama timu zao

BADI MCHOMOLO

ALHAMISI ya wiki iliopita dirisha la usajili nchini England lilifungwa ikiwa ni saa chache kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu.

Wakati dirisha liko wazi timu mbalimbali zilikuwa zinapambana kuhakikisha zinasajili wachezaji ambao walikuwa wanawahitaji kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi. Usajili uliofanywa ni kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao kutokana na mapungufu waliyoyaona msimu uliopita.

Hata hivyo, kuna timu ambazo zimefanikiwa kuzinasa saini za wachezaji ambao waliwakusudia na zipo ambazo zimeshindwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile mchezaji husika kupata majeruhi au bei ya mchezaji huyo kuwa juu.

Mbali na usajili wa Uingereza kufungwa, lakini bado madirisha ya usajili kwa ligi zingine yapo wazi kama vile Hispania, Italia na sehemu zingine, hivyo kuna wachezaji ambao walikuwa na ndoto za kuondoka katika klabu zao za England nafasi hipo.

SPOTIKIKI leo inakuanikia wachezaji wa kiafrika ambao bado wana nafasi kubwa ya kuondoka kwenye klabu zao kutokana na kuhofia kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza au kusumbuliwa na majeruhi.

Henry Onyekuru

Huyu ni mshambuliaji wa timu ya taifa Nigeria, ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Galatasaray kwa mkopo akitokea Everton. Mchezaji huyo bado ana nafasi kubwa ya kuondoka kwenye kikosi hicho kutokana na ugumu wa namba.

Anaweza kujiunga moja kwa moja katika klabu hiyo ya Galatasaray ambayo anaitumikia kwa sasa kwa mkopo. Ugumu wa namba unakuja baada ya Everton kufanikiwa kuinasa saini ya nyota kutoka Arsenal, Alex Iwobi.

Hata hivyo Onyekuru alikuwa anahusishwa kuwindwa na klabu mbalimbali barani Ulaya ikiwa pamoja na mabingwa wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus pamoja na timu ya AS Monaco ya nchini Ufaransa kutokana na kile alichokionesha msimu uliopita katika klabu ya Galatasaray.

Andre Ayew

Msimu uliopita mchezaji huyo alikuwa anakipiga katika kikosi cha Fenerbahce kwa mkopo akitokea Swansea City. Ndani ya kikosi cha Swansea City halikuwa anakosa namba ya kudumu raia huyo kutoka nchini Ghana hivyo akataka kuondoka ili apate timu ambayo atapata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.

Msimu huu mpya wa Ligi atakuwa kwenye kikosi cha Swansea City, lakini nafasi yake ya kucheza itakuwa ndogo kwa kuwa kocha wa timu hiyo Steve Cooper, hana mpango wa muda mrefu na mchezaji huyo kwenye kikosi chake.

Kutokana na hali hiyo, bado mchezaji huyo ana nafasi ya kutafuta timu ambayo anaweza kupata nafasi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la kimataifa.

Eric Bailly

Alikuwa na nafasi kubwa kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United mara baada ya kuwa chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer, lakini bado alionekana kutaka kuondoka kwenye kikosi hicho.

Eric Bailly

Kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita, mchezaji huyo alipata majeraha ambayo yalimfanya akose michezo mbalimbali ikiwa pamoja na michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) nchini Misri wakati timu yake ya Ivory Coast ilipokuwa inashuka uwanjani.

Hata hivyo wakati timu ya Manchester United ikiwa kwenye maandalizi ya msimu mpya, mchezaji hiyo alipata majeruhi mengine hivyo kumfanya awe kwenye wakati mgumu katika kipindi hiki cha msimu mpya.

Anaweza kukosa namba kwenye kikosi hicho kutokana na Manchester United kufanya usajili wa beki aliyevunja rekodi ya usajili Harry Maguire, akitokea Leicester City kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 80.

Hata hivyo kushindikana kwa kuondoka kwa beki wa pembeni wa Man United, Marcos Rojo na ujio wa beki Axel Tuanzebe ambaye alikuwa anakipiga katika kikosi cha Aston Villa kwa mkopo ni wazi Bailly atatakiwa kutafuta timu ya kwenda kuitumikia katika kipindi hiki.

Victor Wanyama

Uongozi wa timu ya Tottenham, umeweka wazi kuwa kiungo wao Victor Wanyama raia wa nchini Kenya, hakuwa kwenye kiwango kizuri msimu uliopita. Alicheza jumla ya michezo 13 ya Ligi Kuu kati ya hiyo alifanikiwa kuwa kwenye kikosi cha kwanza katika michezo minne.

Victor Wanyama

Kutokana na hali hiyo, Tottenham wakaamua kufanya usajili katika kipindi hiki cha kiangazi kwa kuongeza wachezaji katika eneo hilo la kiungo ambalo anacheza Wanyama, wachezaji walioongezwa ni pamoja na Tanguy Ndombele akitokea Lyon na Giovani Lo Celso aliyejiunga kwa mkopo akitokea Real Betis.

Hii itampa wakati mgumu Wanyama kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, hivyo kuna uwezekano wa kutafuta timu ambayo atakwenda kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Yannick Bolasie

Ni nyota wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo pamoja na klabu ya Everton, lakini msimu uliopita alikuwa anakipiga katika klabu ya Anderlecht kwa mkopo. Alitolewa kwa mkopo kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.

Yannick Bolasie

Akiwa na klabu hiyo ya Anderlecht alikuwa kwenye kiwango kizuri, lakini hakuwa kwenye kiwango kizuri wakati wa michuano ya Mataifa ya Afrika nchini Misri, hivyo kocha wa timu ya Everton, Marco Silva aliweka wazi mchezaji huyo hayupo kwenye mipango yake, lakini anatajwa kuwindwa na klabu za Olympique de Marseille na CSKA Moscow.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles