28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mastaa Bongo, majuu walivyosheherekea ‘Valentine’s Day’

SWAGGAZ RIPOTA

KAMA ilivyo kawaida ya kila mwaka inapofika Februari 14, Wapendanao huwa wanaadhimisha kilele cha kuonyeshana matendo ya upendo.

Japo kuwa asilimia kubwa ya watu huiweka siku hii katika upande wa mapenzi huku wengine wakisheherekea ‘Valentine’s Day’ kwa kugusa maisha ya watu wenye uhitaji kwenye jamii.

Swaggaz, tunakukutanisha na mastaa kadhaa wa hapa Bongo na majuu ambao waliitumia siku hiyo kufanya mambo ya upendo kwa wenza wao na watu wanao wazunguka.

SHILOLE, UCHEBE

Kwa sasa Bongo, staa wa muziki Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na mumewe Ashraf Uchebe ni kapo tulivu yenye mvuto wa aina yake kwa mashabiki.

Kwenye siku ya Wapendao, Uchebe aliweka video katika mtandao wa Instagram ikimwonyesha akimpiga busu la mdomo mkewe na kuandika ujumbe wa mapenzi.

“Heri ya siku ya Wapendanao mke wangu Shilole, nakupenda sana, asante kwa kunipenda,” anasema Uchebe.

VANESSA MDEE

Katika siku hiyo ya Wapendanao, nyota wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ambaye yupo kwenye uhusiano wa Jux, alimuuliza mdogo wake Mimi Mars kuwa ni nani atakuwa Valentine wake na Mimi Mars, akamjibu kuwa Valentine wake ni mama yake mzazi.

BARAKA THE PRINCE, NAJ

Licha ya Baraka The Prince kupitia misukosuko ya kukamatwa na polisi kwa madai ya kudhulumu fedha za mrembo anayeitwa Sex Dinah wiki chache zilizopita kisha kuachiwa, yeye na mpenzi wake Naj wameendelea kuonyeshana upendo mkubwa.

 “Ninakupenda kila siku siyo tu Valentine’s Day, wewe ni mtu muhimu kwangu, nafurahi kuwa na wewe siku hii ya Wapendanao,” anasema Baraka.
 
NIKK WA PILI
Miongoni mwa kapo zilizopo juu kwa sasa ni ile ya rapa wa kundi la Weusi, Nikk wa Pili na mchumba wake Joan ambaye kwa sasa ana ujauzito wa miezi sita.
Nikk wa Pili, ametumia ukurasa wake wa Instagram kumtakia heri ya siku ya Wapendanao mchumba wake huyo kwa kuandika: “ Heri ya siku ya Wapendanao Miss Joan, nakupenda mara bilioni na pia nawatakiwa Valentine njema wote wanaopendana kama sisi.”
 

HARMONIZE, SARAH

Kapo nyingine ni ile ya memba wa WCB, Harmonize na Sarah ambao walisheherehkea siku ya Wapendanao wakiwa jijini Dodoma.

“Heri ya siku ya Wapendanao mpenzi wangu Harmonize, asante kwa upendo unaofanya nijisikia vizuri leo, kesho na milele,” anasema mpenzi wa Harmonize.

NAVY KENZO

Kundi hili la muziki linaloundwa na Nahreel na Aika limedumu kwa miaka 11 sasa kwenye mapenzi yao wakiwa wamebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, Gold.

Nahreel ambaye yeye na mpenzi wake wapo Croatia, aliitumia siku hiyo kumnunulia zawadi mbalimbali mpenzi wake ambazo aliziweka katika mtandao wa Instagram na kusindikiza na ujumbe wa mapenzi unaosema.

 “Kila simulizi ya mapenzi ni nzuri lakini yetu ni nzuri zaidi, heri ya siku ya Wapendanao mpenzi wangu Aika,” anasema Nahreel.
 
LULU
Kupitia kampeni ya Save my Valentine, staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, ambayo ilihusisha mashabiki kununua nguo za mwigizaji huyo aliweza kugusa maisha ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu katika vituo vya Faraja House na Tosamaganga Orphanage Centre vilivyopo Iringa.
 
Lulu, anasema aliuza nguo zote 67 alizopanga kuziuza pamoja na kuwashirikisha watu mbalimbali kuunga mkono kampeni hiyo kwa kuchangia nguo, vyakula na fedha.
 

“Ikiwa leo ndiyo hitimisho la kampeni hii napenda kuwashukuru watu wote mlioguswa, watoto hao wamekuwa Valentine wangu kwa sababu kupitia utafiti mdogo nilioufanya nimeona mkoa wa Iringa umekuwa na idadi kubwa ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu,

“Katika kituo cha Tosamaganga Orphanage Centre, kina lea watoto kuanzia mwaka mmoja mpaka mitano na wengi wao mama zao walipoteza maisha wakati wanajifungua, wengine wametelekezwa na wazazi wao wakiwa wadogo,” anasema Lulu.

ZARI APOKEA ZAWADI

Mzazi mwenza wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady  kwa upande wake mambo yalikuwa mazuri, alipokea zawadi ya maua mazuri kutoka kwa mwanamume wake mpya anayemwita King Bae, ambaye muda mfupi ujao atakuwa naye mapumzikoni huko Cape Town , Afrika Kusini.

DIAMOND AMFANYIA ‘SURPRISE’ TANASHA AKIWA STUDIO

Penzi jipya la Diamond Platnumz na mtangazaji wa redio NRG ya Nairobi, Kenya limeendelea kushika chati za wapendanao.

Katika siku ya Wapendanao, Diamond akiwa Dar es Salaam alipanga mpango wa kumshtukiza ‘surprise’ mpenzi wake akiwa kwenye studio za redio hiyo Kenya akiendelea kufanya kipindi.

Tanasha ambaye huwa anatangaza kipindi cha usiku alishangaa watu wengi wakiwa wamebeba maua na bango lililoandikwa ‘I love you Tanasha’, wakiingia studio jambo ambalo lilimshtukiza, akafurahia na kumshukuru Diamond kwa upendo huo.

 “Asante kwa upendo huu mpenzi wangu, mimi ni mwanamke mwenye bahati zaidi duniani kuwa na wewe, maneno hayawezi kuelezea jinsi ninavyojisikia,” alishukuru Tanasha.
 
 

KANYE WEST, KIM KADASHIAN

Mashabiki wanasema, Kanye West ndiyo staa aliyevunja rekodi ya ‘surprise’ siku ya Wapendanao kwa mpenzi wake Kim Kadashian kwa kuweka maua rose sebule nzima na kumualika mpiga saxophone maarufu duniani Kenny G kumburudisha mama watoto wake.

BLAC CHYNA, 6i9INE

Huko majuu nchini Marekani mtandao mmoja wa picha za giza, umesheherekea siku ya Wapendanao kwa kuachia albamu ya muziki  na ndani yake wakiwamo mastaa Blac Chyna na 6i9ine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles