25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 4, 2022

Contact us: [email protected]

Masomo kwa walimu EAC yazinduliwa

Vivienne Yeda
Vivienne Yeda

Na Hadia Khamis, DAR ES SALAAM

BENKI ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB) imezindua mpango wa ufadhili wa masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na hesabu (STEM) kwa walimu ndani ya jumuiya hiyo ikiwa ni mpango wa kuongeza wataalamu katika masomo hayo.

Taarifa hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na  Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Vivienne Yeda.

Alisema mpango huo unaotekelezwa na benki yake kwa kushirikiana na Taasisi ya Africa-America (AAI) ulizinduliwa  Kampala, Uganda hivi karibuni ukihusisha waombaji zaidi ya 300 kutoka   Tanzania, Rwanda, Uganda na Kenya.

“Baada ya mchakato walipatikana washindi watatu, wawili kutoka Uganda na mmoja kutoka Kenya ambao watasafiri mwezi huu kwenda   Marekani   kuanza kusomea shahada za uzamili kwenye Elimu na Hesabu (EDM) kwenye Chuo Kikuu cha Rutgers kilichopo Piscataway, New Jersey.

Aliwataja washindi hao kuwa ni  Emmanuel Nsadha (33) na Theode Niyirinda (31) kutoka  Uganda pamoja na Alfred Mutembei Limbere (26) kutoka Kenya.

“Ufadhili huu umekwenda kwa walimu wazoefu katika ukanda wa Afrika Mashariki pamoja na wahadhiri wenye shahada katika  masomo ya STEM ambao wanafundisha kwenye vyuo vya umma kwenye ukanda huu,’’ alibainisha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Mipango na Maendeleo ya Uchumi wa Uganda, Keith Muhakanizi, aliipongeza benki hiyo kwa jitihada zake za kuleta maendeleo kupitia miradi yake mbalimbali ikiwamo  ya miundombinu na maendeleo binafsi ya watu wa ukanda huo.

“Tunaposherehekea mpango huu ni lazima pia kutambua kwamba faida za udhamini huu haziishii kwa hawa walionufaika tu bali pia unahusisha jamii kwa ujumla.

“Emmanuel, Theode na Alfred watakaporudi  kufundisha katika vyuo vikuu vyao idadi kubwa ya wanafunzi  wao pia watavuna matunda ya mpango huu,’’ alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,544FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles