27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

MASOGANGE ANA KESI YA KUJIBU

MSANII Agnes Gerald maarufu Masogange,  anayetuhumiwa kutumia dawa za kulevya amekutwa na kesi ya kujibu.

Uamuzi huo umetolewa leo Agosti 31, na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Constatine Kakula, kufunga ushahidi wao kwa mashahidi watatu.

Mashahidi wa upande wa Jamhuri waliotoa ushahidi kwenye kesi hiyo ni Mkemia Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye alipima sampuli ya mkojo na maofisa wawili wa polisi ambao walimpeleka Masogange kwa mkemia.

Baada ya kutolewa kwa uamuzi huo, Masogange ambaye anatetewa na Wakili Reuben Simwanza, alidai atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi watatu.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu, kwa ajili ya utetezi na kusema dhamana ya mshitakiwa inaendelea.

Masogange anadaiwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo  yasiyofahamika Dar es Salaam, alitumia dawa  aina ya heroin na Oxazepam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles