27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 10, 2023

Contact us: [email protected]

Maskini Mandojo kumbe ametapeliwa!

Na Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Baada ya Mtanzania Digital kuibua habari ya msanii wa Bongo Fleva Joseph Michael (Mandojo) kuvunjiwa nyumba yake iliyopo Mbweni Maputo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi kwenda kumtembelea nyumbani kwake, leo mkuu huyo ameendesha kikao cha majadiliano na ambacho hata hivyo suluhu yake inatarajiwa kutolewa kesho kutwa.

Taarifa za ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na mkuu wa Wilaya hiyo ofisini kwake leo kimegundua kwamba msanii huyo alitapeliwa kwa kuuziwa kiwanja hicho na watu wasio wamiliki halali.

Aidha mkuu huyo wa wilaya amewataka polisi Kinondoni waendelee kuwasaka wote walioshiriki kumuuzia msanii huyo kiwanja ilihali wakijua kwamba wao sio wamiliki halali.

Awali Hapi alipokuwa ametembelea nyumbani kwa msanii huyo alilitaka jeshi la polisi Kinondoni kuwatafuta watu hao lakini hadi leo walipokutana na msanii huyo pamoja na waliovunja nyumba yake kujadili kwa pamoja bado hawajapatikana.

“Watu hawa waliomuuzia Mandojo kiwanja ilihali wakijua wao sio wamiliki halali wajisalimishe wenyewe na wasipofanya hivo namuagiza RPC  wakamatwe ndani ya saa 48 na taarifa niletewe ofisini kwangu hawawezi kuturudisha kule tulipotoka,”amesema Hapi.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,414FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles