24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Maskini Coutinho, Kakutwa na nini pale Barcelona?

ADAM MKWEPU NA MITANDAO


KOCHA wa Bracelona, Ernesto Valverde, ndiye anayekiongoza kikosi maalumu katika mpango wa kunusuru kipaji cha Philipe Coutinho pale Barcelona.


Wote Valverde na msaidizi wake, Jon Aspiazu, wanaendelea kuamini kuwa kuna siku Coutinho atarejea katika kiwango chake bora.


“Unataka kusema kitu gani kuhusu Philippe?Kila wakati anajaribu kufanya aliwezalo kujaribu kurejea katika kiwango chake, kurejesha imani ya watu wake,”anasema Valverde.


“Kila wakati anajaribu kufanya kitu cha ziada, hicho ni kitu bora kwetu,”anaongeza Kocha Msaidizi.
Valverde anayaeleza hayo baada ya kuulizwa kuhusu kiwango kibovu cha Coutinho alichokionyesha katika mchezo uliochezwa wiki iliyopita dhidi Girona.


Katika mchezo huo Coutinho alikosa kufunga akiwa yeye na kipa.
Lakini Valverde hakumtoa nje ya uwanja na amefanya hivyo katika michezo minne iliyopita ya Ligi Kuu Hispania licha ya kiwango kibovu anachokionyesha nyota huyo ambaye alisajiliwa kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi akitokea klabu ya Liverpool.


Coutinho alipomzishwa katika mchezo wa Kombe la Mfalme wiki iliyopita na kutumika kama mchezaji wa akiba katika mchezo dhidi ya Sevilla ambao nao alionyesha kiwango kibovu licha ya kupata nafasi mara kadhaa.


Lakini pamoja kuwepo katika uangalizi maalumu kumekuwapo na hadithi ya nyota huyo kutaka kuondoka kurejea Ligi Kuu England ingawa klabu ya Barcelona imeonyesha haina mpango wa kufanya hivyo kwa sasa.
Klabu hiyo inafikiria kumbakisha nyota huyo na kumfanya kuwa sehemu muhimu katika kikosi cha baadae cha timu hiyo.


Ikiwa klabu inaweza kuzuia biashara hiyo isifanyike basi kikwazo kikubwa kinaweza kuwa namna ya kuamua jukumu la nyota huyo anapokuwa ndani ya uwanja.


Coutinho alisajiliwa kurithi mikoba ya aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Andrea Iniesta, lakini inaonekana Arthur Melo amekuwa akilingana kiuchezaji na kiungo huyo aliyeamua kustaafu kuchezea timu hiyo.
Ujio wa Frenkie de Jong katika nafasi ya Coutinho unaondoa uhakika wa nafasi yake katika kikosi hicho hapo baadae.


Kwa sasa Coutinho ni mchezaji wa tatu katika sehemu ya mbele ya timu hiyo lakini kurejea kwa Ousmane Dembele baada ya kupona jeraha lake hivyo anaweza kuichukua nafasi hiyo.


Kocha Valverde anaamini Coutinho anaweza kuimarika katika eneo la kati ili kuboresha thamani yake kwa timu katika idara hiyo, na kwamba hutoa kitu tofauti na Dembele katika mashambulizi.


Kiungo huyo alionekana kuwa bora wiki mbili zilizopita wakiwa uwanja wa nyumbani Camp Nou dhidi ya Eibar akitoa pasi mbili za mabao katika dakika 90 alizocheza.


Kiwango chake kimesahaulika kwa sababu hakifanani na hadithi yake iliyomfanya asajiliwe kwa kiasi kikubwa cha fedha kabla.
Lakini ipo wazi ni kwamba mchezaji huyo aliyesajiliwa na Barcelona kwa pauni milioni 142 akitokea Liverpool hafai kuonekana katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kwa sasa kutokana na kiwango chake.


Ingawa kiwango kinakuja na kuondoka, kocha Aspiazu anasema: “Labda Coutinho hayupo sawa kama msimu uliopita lakini kwa sasa kidogo amezidiwa hata na Ousmane Dembele.”


Lakini hata kama anacheza ndani kidogo hivi karibuni Dembele yupo vizuri na Coutinho anaonekana kama mchezaji ambaye hawezi kuchukua nafasi ya Iniesta kwa muda mrefu wala nafasi ya Neymar ambaye alijiunga na klabu ya Paris Saint Germain (PSG).


Uimara wake wa kumiliki mpira wakati mwingine unaweza kumfanya Dembele kuwa kipaumbele hasa katika mfumo unaohitaji msaada wa mbio zake .
Javier Mascherano anasema: “Nilipaswa kujifunza jinsi kucheza soka Barcelona.”


Hiyo inaweza kuwa haitoshi kamwe kuhalalisha bei iliyopoteza Barcelona lakini wanafahamu kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 26 na mkataba hadi mwaka wa 2023 bado ana muda wa kujifunza mengi ndani ya klabu hiyo.


Coutinho alisajili Janauri mwaka jana wakati Iniesta alipokuwa Barcelona, Valverde alitakiwa kumjaribu katika nafasi nyingine katikati ya kampeni za Ligi Kuu Hispania ambayo kwa raia huyo wa Brazili ingemjenga kabla.


Katika michezo 16 ya La Liga, nyota huyo alicheza mara 5 kama winga wa kulia, na mara 6 upande wa kushoto. Katika michezo muhimu zaidi, Coutinho alicheza katika jukumu ambalo mara chache upenda kucheza.Upande wa kulia.


Dhidi ya timu kama Atletico Madrid, Real Madrid na mchezo wa Copa del Rey dhidi ya Sevilla alianza akitokea upande wa kulia.


Pamoja na kuondoka kwa, Andrés Iniesta, kujiunga na klabu ya Vissel Kobe, wakati ulifika kwa Coutinho kucheza nafasi ya kushoto.
Hii ndio jinsi kampeni hii ilianza, na mechi dhidi ya Valladolid, Huesca na Leganés za La Liga, na dhidi ya PSV katika Ligi ya Mabingwa Ualaya Uwanja wa Camp Nou.


Barcelona ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya Leganes, Coutinho akionyesha kiwango duni eneo la katikati dalili ambazo hazikuwa njema kwa timu hiyo yake na Valverde aliamua kumuondoa.


Tangu hapo Coutinho hajawahi kucheza tena katika eneo hilo.
Katika michezo tisa ya Ligi Kuu tangu mwanzo Coutinho alikuwa akicheza akitokea kushoto.


Pia katika michezo mitano iliyopita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na katika Copa dhidi ya Levante. Katika hali hii, na Dembélé kuwa katika kiwango bora, Coutinho lazima atasubiri baada ya kurejea kwa Mfaransa huyo.


Katika bodi ya wakurugenzi kuna wasiwasi kuwa Valverde anataka kucheza kamali kuhusu Coutinho ili kucheza nafasi aliyosajiliwa, na kuweka historia ndani ya klabu hiyo.


Kocha hakuweza kumhamasisha mchezaji na kumfanya awe na msimamo zaidi mahali ambapo anahitaji kucheza. Coutinho, kama kiungo, anatakiwa kuisaidia Barcelona kumiliki mpira.


Coutinho aonyeshi kuufurahi mpira kama alipokuwa Liverpool ambako alikuwa akifanya vizuri chini ya kocha Jurgen Klopp.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles