25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MASKINI AVEVA……!

1Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya soka ya Simba, imedaiwa kumponza Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, kwa kufanya uamuzi ambao umemtia matatani na kuwa chini ya uchunguzi unaofanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru).

Kamati hiyo ilidaiwa kuamua kutumia akaunti binafsi ya kiongozi huyo kwa ajili ya malipo ya mchezaji wao wa zamani, Emmanuel Okwi ya shilingi milioni 450 za Tanzania, yaliyofanywa na klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia iliyomsajili nyota huyo Januari 2013, wakati klabu hiyo ikiwa chini ya Mwenyekiti Ismail Aden Rage.

Kaimu Msemaji wa Takukuru, Tunu Mleli, alinukuliwa jana akisema kwamba, kilichomfanya kiongozi huyo achunguzwe ni tuhuma za uchepushwaji wa fedha za Okwi.

“Ni kweli Aveva amekamatwa na polisi baada ya Takukuru kuagiza hivyo kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili, ikiwa ni pamoja na uchepushwaji wa fedha kutoka akaunti ya Simba kwenda katika akaunti yake binafsi na baadaye kuanza kufanyiwa mgawanyo katika akaunti nyingine,” alisema Mleli.

Awali alipoulizwa na MTANZANIA Ofisa Habari wa Takukuru, Musa Milaba, alisema kwamba bado hajui lini watamwachia kiongozi huyo kwa kuwa yupo kwa ajili ya uchunguzi.

“Tunamshikilia na yupo kwenye mikono salama. Sisi tunaendelea na uchunguzi wetu, sheria inaturuhusu kufanya uchunguzi, tunaruhusiwa kukamata, kupekuwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo inasema kwamba uamuzi huo wa kutumia akaunti ya Aveva kulipwa fedha za Okwi, ulipewa baraka na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo.

“Tangu jana (juzi) usiku Aveva yupo chini ya ulinzi wa polisi Kituo cha Urafiki Dar es Salaam, bila ya taarifa rasmi ya kukamatwa kwake lakini inawezekana sababu ya kuwapo huko inatokana na fedha za malipo ya Okwi ambazo zilionekana hazina maelezo.

“Na kama ikiwa ni kweli, si kosa la Aveva kwa sababu uamuzi huo haukuwa wake pekee kwani Kamati ndiyo ilifanya uamuzi huo,” kilisema chanzo hicho.

Aidha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Chistopher Fuime, alithibitisha kumshikilia kiongozi huyo, huku akidai kwamba Takukuru ndio wanaojua tuhuma zinazomkabili kiongozi huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles