Mashinji, viongozi saba wakamatwa kwa amri ya DC Sabaya

0
969

Upendo Mosha, Hai

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Vincent Mashinji na viongozi wengine wa chama hicho saba wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro wakati wakiendelea na kikao cha ndani maeneo ya Bomangombe wilayani Hai kwa amri ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Lengai ole Sabaya.

Katibu wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Basil Lema, amethibitisha kushikiliwa kwa viongozi hao, ambapo amesema walikamatwa leo Jumamosi Desemba 29, saa sita mchana katika ukumbi mmoja mjini hapa wakati wakiendelea na kikao chao cha ndani

”Kabla ya kukamatwa kwa viongozi hao, Mkuu wa Wilaya Sabaya, alituandikia barua ya kuzuia kikao hicho jambo ambalo ni kinyume cha sheria”, amesema

.Hata hivyo, Sabaya amethibitisha kutoa maagizo ya kukamatwa kwa viongozi hao kwa madai kwamba hawakufuata taratibu  na kwamba uongozi wa wilaya ulikuwa hauna taarifa.

“Ni kweli nimeagiza viongozi hao wa Chadema wakamatwe akiwamo huyo kinara wao ambaye ni Katibu Mkuu wao na nilitumia dola ili niwakumbushe kuwa kila kitu kinafuata taratibu na Wilaya ya Hai si sehemu ya kuja kuzurura na kufanya wapendayo”, amesema Sabaya.

ReplyForward

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here