25 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Mashinji huyooo CCM, adai Chadema bado wako mbali kimaendeleo

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Vincent Mashinji ametangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo Februari 18, Lumumba jijini Dar es Salaam.


Dk. Mashinji ametangaza uamuzi huo ikiwa ni siku nane baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye atangaze kurudi CCM na siku tatu baada ya Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe ahamie CCM.


Kwa kauli yake Dk. Mashinji amesema kilichomsukuma kuhamia CCM ni baada ya kutafakari mwenendo mzima wa siasa na uchumi nchini na kuangalia kina nani wako tayari akaona kwa upande wao Chadema bado wako mbali sana katika kuchochea mambo ya maendeleo.


“Tanzania haiumbwi na malaika bali binadamu na wanatofautiana, nimeona wenzetu wa CCM wanasikiliza sasa nikaona ni heri nije niongee na wenzangu nione kama nitapata fursa ya kutoa mchango kwenye taifa langu.


“Miaka 47 bado ni kijana kama rais Magufuli anavyosisitiza maendeleo hayana chama hivyo nimuombe Mwenyekiti wa CCM kama ataridhia anikubalie nijiunge na chama hiki.


“Ninaona CCM iko tayari iko tayari kuwaendeleza Watanzania na kule nilikotoka huu utayari bado sijauona,” Dk. Mashinji ambaye alipokelewa na Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole.


Akizungumza baada ya kumpokea Dk. Mashinji, Polepole amesema anaelekeza ngazi inayofuata uiweke utaratibu mahsushi kusajili uanachama wake kwa mujibu wa katiba ya CCM.


Nchi hii inahitaji watu wengi zaidi ambao wana uchungu na maendeleo ya Watanzania ambao wanatambua ya kwamba tumechelewa. CCM imepewa dhamana kipindi hiki na Watanzania itoe maendeleo.


“Basi tukiungana pamoja tukapiga hatua kubwa basi nina hakika kwa maneno haya uliyosema Tanzania itapiga hatua kwa haraka na maendeleo ambayo Watanzania wanayatarajia yatakuja kwa haraka zaidi,” amesema Polepole.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,540FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles