MASHINE ZA EFD ZATENGAMAA

0
849

Elizabeth Hombo, Dodoma           |     


Wafanyabiashara wametakiwa kurejea kutumia mashine za kieletroniki (EFD) kwa kuwa hitilafu iliyokuwa imetokea imetatuliwa.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo jioni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia kwenye bajeti ya wizara yake.

“Baada ya kutokea hitilafu iliyosababisha kifaa kilichokuwa kinatunza na kuchakata taarifa za wafanyabiashara kuharibika tayari imetatuliwa na wataalamu wetu wa teknolojia na mawasiliano.

“Tangu Juni Mosi mwaka huu wataalamu walifanikiwa kurejesha kwenye hali ya kawaida na kufanya kazi kama awali.

“Tatizo lililotokea kwa kujua au kwa kusudi, hata baada ya mfumo kurudi katika hali ya kawaida baadhi ya wafanyabiashara walizima mashine zao.

“Wito wangu kwa wafanyabiashara warejee kutumia mashine za EFD na tangu jana nimetoa maagizo kwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nchi nzima kuwatembelea wafanyabiashara wote kama mashine zao zinafanya kazi,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here