23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mashine ya MRI Muhimbili yaharibika tena

mictuVeronica Romwald na Allen Msapi (GHI), Dar es Salaam

MASHINE ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ijulikanayo kama Magnetic Reasonance Imaging (MRI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, imeharibika tena baada ya kufanya kazi kwa siku mbili, tangu ilipofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Philips.

Mashine hiyo ilifanyiwa matengenezo kutokana na shinikizo la Rais Dk. John Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo na kuamuru zifanyiwe marekebisho haraka.

Katika ziara yake hiyo, Dk Magufuli alishangaa kuona wagonjwa wamekaa hospitalini hapo kwa zaidi ya miezi miwili bila kutibiwa, kutokana na mashine hiyo kuwa mbovu.

MRI ni mashine inayotumia sumaku kupiga picha badala ya mionzi. Wataalamu wa masuala ya afya wanasema ni mashine ambayo inapiga picha zenye ubora zaidi kuliko zilizopigwa na mashine ya CT Scan.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja, Aminiel Aligaesha, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa, huduma za uchunguzi zinazofanywa na mashine hiyo zimesitishwa hadi hapo itakapotangazwa tena.

“Mapema wiki iliyopita tuliwatangazia wananchi kwamba huduma za MRI zimeanza kutolewa baada ya mashine hiyo kutengenezwa. Katika taarifa hiyo tuliwaeleza kuwa matengenezo ya kifaa kingine cha CT- Scan yalikuwa yakiendelea.

“Hata hivyo baada ya mashine ya MRI kufanya kazi Novemba 11 na 12, mwaka huu ilionekana kuna hitilafu ya kiufundi ambayo inahitaji matengenezo zaidi hali iliyotulazimu kusimamisha kufanya kazi kuanzia Novemba 13 mchana,” alisema.

Alisema uongozi wa hospitali hiyo umeshawasiliana na kampuni ya Philips ambayo ina mkataba wa kuzifanyia matengenezo mashine hizo ili kurekebisha hitilafu zilizojitokeza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles