MASHAMBULIZI YA SUMU YAUA 100 SYRIA

0
547

DAMASCUS, SYRIA

WATU 100 wakiwamo watoto 25, wamekufa nchini Syria kufuatia mashambulizi ya kemikali zenye sumu katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi.

Kwa mujibu wa Rami AbdelRahman wa Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria lenye makao yake Uingereza, mashambulizi hayo yaliyotokea eneo la Kaskazini Magharibi mwa Syria, yalitumia gesi ya sumu iliyosababisha baadhi ya watu kubanwa na pumzi, kutapika na wengine kutokwa na mapovu midomoni.

Mashambulizi hayo yametokea eneo la Khan Sheikhoun katika Jimbo la Idlib.

Mjini New York, Umoja wa Mataifa (UN) umelaani mashambulizi hayo, na msemaji mkuu wa umoja huo, Stephane Dujjaric, aliwaambia waandishi wa habari kuwa ripoti za aina yoyote za matumizi ya silaha za kemikali, hasa dhidi ya raia ni za kutisha sana.

Alisema matumizi ya silaha za kemikali popote ni tishio kwa amani na usalama wa kimataifa na ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here