23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Mashambulio yaongezeka kati ya Israel na Hamas

Gaza, Israel

Israel na kundi la Hamas la Palestina zimetumia silaha nzito nzito wakati ghafla mashambulio yyamegeuka kua mabaya Jumatatu usiku kati ya wahasimu wawili wakuu wa Masharki ya Kati, na kusababisha vifo vya watu 28.

Ghasia zilizoanza kwenye mji wa Jerusalem zimenea sehemu nyingi za Israel na mashambulio ya roketi na makombora kati ya Hamas na jeshi la Israel.

Mataifa makuu ya dunia yanatoa wito wa utulivu kurudi tena, huku nchi za Kislamu zikeleza hasira kutokana na kuongezeka kwa ghasia kuwahi kushuhudia kwa miaka kadhaa pale wapiganaji wa Hamas kutoka Ukanda wa Gaza wakifyetua msururu wa roketi, huku taifa la Kiyahudi likishambulia kwa ndege za kijeshi na helikopta

Kwa upaande wa wapalestina, watoto tisa wameuliwa mionngoni mwa watu 26 walouwawakatika Ukanda ulofungwa wa Gaza na watu 125 kujeruhiwa.

Kwa upande wa Israel roketi zimewauwa wanawake wawili wa mji wa Ashkelon, kaskazini mwa Gaza ambako wapiganaji wa hamas wamefyetua roketi 100.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya Jumanne kwamba Jeshi la Ulinzi la Israel litazidisha hivi sasa mashambulizi yake, ambayo jehsi linasema limesha haribu vituo vya kijeshi na kuwauwa makamanda 17 wa Hamas.

Kufikia leo mchana kundi la wanamgambo la Hamas linalotawala kanda ya Gaza limefyetua zaidi ya roketi 300 kuelekea mji wa Jerusalem ambapo waisraeli wanasema asili mia 90 za roketi hizo zimezuiliwa na mfumo wa ulinzi wa makombora maarufu kama Iron Dome.

Israel kwa upande wake imejibu kwa kufanya mashambulio 130 ya makombora hadi Gaza na kusababisha uharibifu mkubwa.

Netanyahu aonya kufanya mashambulizi zaidi

Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu alisema jana usiku kwamba wanashambuliwa kutoka kila pembe na watajibu vikali.

Usiku wa leo siku ya Jerusalem, makundi ya kigaidi huko Gaza yamevuka mstari mwekunduna kutushambulia kwa makombora nje yam ji wa Jerusalem. Israel itajibu kwa nguvu zote. Hatuta stahmilia mashambulio kwenye ardhi yetu, kwenye mji mkuu wetu, dhidi ya wananchi na wanajeshi wetu.

Roketi na makombora yalipokua yanafyetulwa, Wapalestina walikua wanapambana na maafsa wa usalama kwenye uwanja wa mskiti wa Al Aqsa ambako watu kadhaa walijeruhwa. Maafisa wa Afya mjini Jerusalem wanasema watu kadhaa wamepoteza macho yao baada ya kupigwa na risasi za mpira zinazofyetuliwa na polisi wa Israel.

Upande wa pili wa mskiti huo waumini wamekua wakimba na kuomba dua kuunga mkono vita vya wapalestina.

Kulikua pia na mabambano katika miji mingine ya Israel ikiwemo Bethlehem pamoja na kituo cha ukaguzi cha Qalandia kati ya mji wa Ukingo wa magharibi wa ramal ana Jerusalem.

Kuongezeka kwa ghasia kunaendelea kuzusha wasi wasi kote duniani. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kupitia msemaji wake Stephane Dujarric kwamba anafutilia kwa makini na kwa wasi wasi kuzorota kwa hali ya usalama huko Mashariki ya kati.

wasi wasi unaongezeka kwenye Jumiya ya Kimataifa

Viongozi wa nchi za kiarabu wametoa taarifa kulaani uvamizi wa mskiti wa Al Aqsa ulofanywa na maafisa wa usalama wa Israel, pamoja na mashambulizi ya makombora na roketi..

Waziri wa mamabo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken alipokua anakutana na waziri mwenzake wa Jordan Ayman Safad Jumatatu mchana amesema wana fuatla kwa wasi wasi mkubwa na kwamba ni lazima mashambulzi ya roket na makombora yasitshwe mara moja.

“Pande zote zina bidi kuacha mashambulzi, kupunguza mvutano na kuchukua hatua za kurudisha utulivu. Na kwa mara ningine ninasema nina wasi wasi mkubwa kuhusu mashambulizi ya roketi na kila upande uchukuwe hatua kusitsha hali hii.”.

Nae msemaji wa White House Jen Psaki anasema utawala wa Biden unafuatilia kwa karibu ghasia zinazoendelea huko Israel.

Ghasia zikiendelea maandamano ya kuwaunga mkono wapalestina yanafanyika huko Lebanon, Uturuki, Toronto Canada, Morocco na kwengineko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,303FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles