23.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Mashabiki West Ham wawashambulia Man United

west-ham-manMANCHESTER, ENGLAND

BASI la klabu ya Manchester United lilishambuliwa kwa mawe lilipokuwa linaelekea katika Uwanja wa Upton Park ambao unamilikiwa na wapinzani wao, West Ham.

Mashabiki wa West Ham walikuwa wanalisubiri basi hilo wakati linaelekea uwanjani hapo kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu nchini England katika mchezo ambao ulimalizika kwa United kupokea kichapo cha mabao 3-2 na kuifanya klabu hiyo ishuke ‘top four’.

Shambulizi hilo lilisababisha mchezo huo baina ya Manchester United na West Ham kucheleweshwa kwa zaidi ya dakika 45.

Mchezo huo ulikuwa umeratibiwa kuanza saa tatu na dakika 45 usiku, lakini ukaanza saa nne na nusu, hivyo kuwafanya Man United waupoteze.

Hata hivyo, madirisha ya basi hilo yalivunjwa na mashabiki hao ambao walikuwa wanarusha mawe na chupa za bia ila askari walipambana na ghasia hizo kwa ajili ya kuwalinda na kuwasindikiza wachezaji hadi uwanjani.

“Ilikuwa tukio la kushtua sana, haikufurahisha kabisa kushambuliwa na mashabiki wa timu pinzani hadi gari letu linaharibiwa,” alisema nahodha wa Manchester United, Wayne Rooney.

Hata hivyo, kocha wa Man United, Van Gaal, aliweka wazi kwamba timu yake ilipoteza mchezo huo kutokana na wasiwasi za mashabiki ambao walionekana uwanjani hapo wakiwa na hasira.

Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa West Ham kuutumia uwanja huo kwa michezo yao ya nyumbani kwa kuwa inatarajia kuhamia makao yao mapya ya Olympic Stadium. West Ham imekuwa ikiutumia uwanja wa Upton Park kwa miaka 112 sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles