Mashabiki wakerwa na Kanye West

0
1161

NEW YORK, MAREKANI


MASHABIKI wa mwanamuziki wa Marekani, Kanye West, wamekerwa na  kitendo cha mwanamuziki huyo kushindwa kutimiza ahadi yake ya kuachia albamu mpya ya Yandhi wiki iliyopita.

Kutokana na kitendo hicho, Jumamosi iliyopita Kanye West alitarajiwa kutoa maelezo kuhusu kuchelewa kwa albamu hiyo japo hakufanya hivyo.

Septemba 21, mwaka huu, Kanye aliandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa albamu yake mpya ataiachia Septemba 29, mwaka huu na kushindwa kufanya hivyo.

Lakini kitendo hicho kiliwafanya mashabiki wa nyota huyo mtandaoni kuhitaji majibu kuhusu kuchelewa kuachiwa kwa albamu hiyo.

Wakati mashabiki wa Kanye wakisubiri nyota huyo kudondosha albamu yake mpya, muda huo huo ndipo mwanamuziki Lil Wayne alipoachia albamu mpya ya Carter V ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here