22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Mashabiki wa Liverpool wanavyomlia ‘denge’ Klopp

Jurgen Klopp
Jurgen Klopp

Na ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM

NI kwa muda gani wanatakiwa kusubiri kabla hawajapoteza imani kwa kocha wao? Ni muda gani timu itaonekana ikicheza kwa kiwango bora?

Hayo ni maswali mawili ambayo si rahisi kupata majibu yake na kila swali moja  linaonekana kuanza kuwachanganya si mashabiki wa timu ya Liverpool bali hata uongozi wa klabu hiyo.

Iangalie vema Liverpool, Jumamosi iliyopita Jurgen Klopp alirejea uwanja wa White Hart Lane  unaotumiwa na timu ya Tottenham Hotspurs  ambapo Oktoba mwaka jana waliambulia kichapo ukiwa ndio mchezo  wa kwanza wa kocha huyo.

Watu wengi wanaamini Liverpool ilifanikiwa kufanya mapinduzi ya kumwajiri kocha huyo bora Ulaya.

Miezi tisa tu Klopp akiwa katika jiji la Liverpool, amekuwa maarufu zaidi alivyokuwa katika timu ya Borussia Dortmund.

Kocha huyo amesaini mkataba mrefu unaomfanya atambe katika klabu hiyo hadi mwaka 2022.

Kama kulikuwa na sauti pinzani katika timu hiyo basi zimekuwa kimya na kubaki chache tangu ujio wa kocha huyo.

Chini ya uongozi wa Klopp, Liverpool imeweza kuwa na uwiano wa ushindi 1.59 kwa kila mchezo ambapo wakati wa kocha Brendan Rodgers timu hiyo ilikuwa na uwiano wa ushindi wa 1.88 kwa kila mchezo.

Hesabu hizo hazielezi wala kutoa majibu ya kila kitu, kwani kumekuwapo na mkanganyiko wa hoja kwamba Klopp anaendeleza matatizo yaliyoachwa na mtangulizi wake.

Kwa kufanya hivyo, Klopp anadaiwa kuirudisha timu hiyo kwenda nyuma badala ya mbele.

Katika mahojiano ya gazeti la Stern, Klopp alielezea njia anayotumia kununua wachezaji wa kawaida badala ya wale wa gharama ambao aliwafananisha na ugonjwa.

Hata hivyo, ubora wa kikosi cha Liverpool akihitaji haraka ili ubora wake kuonekana ingawa Klopp anatakiwa kuwa mpole kusubiri matokeo ya kile anachokifanya.

Kwa njia nyingine, kinachofanyika na kocha huyo bado kinapokelewa kwa furaha na mashabiki wa timu hiyo.

Lakini aina au mtindo wa Klopp unawafanya mashabiki wa timu hiyo kuwataka wachezaji kuipigania timu hiyo haraka kabla ya mambo hayajaharibika.

Kwani jambo kama hilo liliwahi kutokea kwa kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ambaye alilalamikiwa katika kipindi cha runinga cha Reality TV kwamba mtindo wa uchezaji wa timu yake ulikuwa ukiwaudhi mashabiki hao.

Klopp bado anaonekana kuwapa matumaini mashabiki wa timu hiyo kutokana na mafanikio yake akiwa klabu ya Mainz na Borussia Dortmund.

Wakati Liverpool ilipokuwa bora ilikuwa imara sawa sawa ikikumbukwa katika msimu uliopita ushindi wa michezo miwili dhidi ya Manchester City au ubora ulionekana katika michezo miwili ya Ligi ya Europa dhidi ya Villarreal na Dortmund.

Zaidi ya hapo soka linasukumwa na presha ya mashabiki wakitaka kufanya vizuri bila ya kuyumbishwa kwani Liverpool kama ingeweza kufanya vizuri kama ilivyofanya katika michezo hiyo ingekuwa bora zaidi duniani.

Lakini timu hiyo imeshindwa kuwa katika msimamo imara katika michezo yake bila kupata matokeo ya kutia shaka.

Kwani kwa sasa timu hiyo inaweza kucheza vizuri na kuvutia ndani ya dakika 20 tu za mwanzo baada ya hapo inapotea kabisa ndani ya dakika 70 uwanjani.

Hilo lilitokea hata katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu England, ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Arsenal ambapo kipindi cha kwanza kilitosha kuwapa ushindi huo lakini dakika zilizobakia zilikuwa hazina mvuto kutokana na uchezaji wao.

Kasoro hiyo ilijitokeza pia  katika mchezo wa pili dhidi ya Burnley ambapo Liverpool ilifungwa mabao 2-0.

Inafahamika kwamba, Liverpool wanaweza kushambulia iwapo wapinzani wao watafanya hivyo kwa kuwaachia mwanya wa kuwashambulia.

Kwa sasa Liverpool wanaweza kuwa na nguvu katika mchezo lakini wasipende kupambana.

Wanapokwenda kushambulia swali pekee unaloweza kujiuliza je, safu yao ya ulinzi inaweza kuzuia wasifungwe? Je, wanaweza kuvunja safu ya nyuma ya wapinzani wao na kucheza kwa kukabia chini ya dimba na vipi wanaweza kumfanya Jordan Henderson kuwa Sergio Busquets?

Inawezekana kwamba matokeo ya mchezo dhidi ya Burnley yamewashtua lakini kama timu hiyo haitakuwa tofauti na msimu uliopita itakuwa ngumu kwa mashabiki wa timu hiyo kuwa na uvumilivu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles