25.5 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Mashabiki Villa: Samatta baba lao

London, England

LICHA ya kucheza dakika 66 pekee katika mchezo wa usiku wa kuamkia jana dhidi ya Leicester City, mwanasoka wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta, amefanikiwa kuwateka mashabiki wa Aston Villa.

Katika mchezo huo wa marudiano ya nusu fainali ya Kombe la Ligi, Samatta alikuwa sehemu ya kikosi chake kwanza, huku Villa wakishinda mabao 2-1 kupitia kwa Matt Targett na Mahmoud Hassan ‘Trezeguet’.

Samatta alikaribia kuzitikisa nyavu za Leicester wakati Villa wakiwa wanaongoza bao 1-0 lakini alishindwa kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Jack Grealish.

Nyota huyo aliyetua Villa akitokea Genk alikaribia tena kuwatungua Leicester katika dakika ya 26 lakini alishakuwa kwenye eneo la kuotea wakati anapokea pasi ya Frederic Guilbert.

Akimzungumzia Samatta aliyeitwa benchi katika dakika ya 66 na nafasi yake kuchukuliwa na Keinan Davis, mmoja kati ya mashabiki wa Villa, Ash, alitumia ukurasa wake wa Twitter kuandika: “Nimeona kitu kwa Samatta, ni mzuri. Alitakiwa kuondoka na bao lakini apewe wiki chache na hakika tutaona mabao yake.”

Shabiki mwingine, Alex Franklin, aliandika: “Ni mwanzo mzuri kwa Samatta. Nimekoshwa na hilo. Hakuna kinachoweza kunipa hofu kwa alichokionesha.”

Dale Wootton ni shabiki wa Villa pia, naye aliandika: “Nilichokiona kwa Samatta kinaniambia atafunga mabao mengi.”

Jumamosi ya mwishoni mwa wiki hii, Samatta atacheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya England akiwa na Villa, endapo kocha wake, Dean Smith, atampa nafasi dhidi ya Bournemouth.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles