26.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Maseneti wamnyoshea kidole mfalme wa Saudia mauaji ya Khashoggi

WASHINGTON DC, Marekani



MASENETI wa Bunge la Seneti nchini hapa wamenyooshea kidole Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman wakisema kuwa hawana shaka alihusika  katika mauaji ya mwanandishi wa habari,  Jamal Khashoggi.

Baraza hilo sasa   linapanga kupigia kura mapendekezo ya kusitisha uungaji mkono kijeshi wa Marekani kwa Saudia na washirika wake katika vita inyoendelea Yemen.

Taarifa zilizopatikana mjini hapa zinaeleza kwamba tayari wajumbe wa vyama vyote viwili vya Democrat na Republican wameshakubaliana katika hatua ya mwanzo ya pendekezo hilo.

Msimamo huo wa maseneta unakuja baada ya kufanya kikao cha siri na Mkuu wa Shirika la Ujasusi la hapa, CIA,  Gina Haspel.

Katika msimamo wao huo, Seneta wa mwenye ushawishi mkubwa kutoka Chama cha Republican,  Lindsey Graham alisema ana imani ya hali ya juu kuwa Bin Salman, alipanga njama ya kumuua Khashoggi.

Seneta huyo wa jimbo la Carolina Kusini alisema Bin Salman ni mwendawazimu na n mtu hatari.

Khashoggi aliuawa ndani ya ofisi za ubalozi mdogo wa Saudi Arabia jijini Istanbul, Uturuki Oktoba 2 mwaka huu.

Mwanahabari huyo alikuwa ni mkosoaji mkubwa wa sera za Saudia hususani mwanamfalme Bin Salman.

Tayari Saudia imewashitaki watu 11 juu ya mauaji hayo, lakini wanakanusha vikali juu ya uhusika wa Bin Salman.

Mkurugenzi wa CIA, Haspel alikutana juzi na wajumbe wa Seneti wa Kamati ya Mambo ya Nje ambao hawakumung’unya maneno baada ya mkutano huo.

“Hapa hakuna bunduki inayofuka moshi – kuna msumeno unaofuka moshi,” alisema Seneta Graham akimaanisha mauaji ya Khashoggi yanayodaiwa kutekelezwa kwa kumny’onga kisha kumkata mwanahabari huyo vipande kwa kutumia msumeno.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles