22.9 C
Dar es Salaam
Monday, September 9, 2024

Contact us: [email protected]

Masele ataja sababu za kuwasiliana na Rais

Ramadhan Hassan,Dodoma

MAKAMU Mwenyekiti wa Bunge la Afrika (PAP) na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele, ameeleza sababu zilizomfanya awasiliane na Rais ,Waziri Mkuu baada ya kupokea barua ya Spika wa Bunge Job Ndugai iliyotaka kumvua madaraka katika Bunge la Afrika.

Masele Jumatatu alihojiwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutokana na maagizo ya Spika Ndugai kwamba ahojiwe kutokana na kufanya utovu wa nidhamu katika Bunge la Afrika.

Akizungumza leo Mei 23 bungeni mara baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuwasilisha taarifa yake, Masele amesema barua aliyoituma Spika Ndugai kwa Rais wa Bunge la Afrika, Roger Dang ilitaka kumvua madaraka.

“Mheshimiwa Spika, Rais wa Bunge la Afrika aliitumia hii barua yako kutaka kunivua madaraka ya uongozi wa Bunge la Afrika kwa kuzingatia barua yako Mheshimiwa Spika wangu ninayekuheshimu, nilitafakari sana kwa haraka nifanye nini kwa maslahi ya Taifa langu nifanye nini kwa maslahi yangu mimi binafsi kama kijana ninayekuwa katika uongozi.

“Nilifikiria haraka na burasa yangu iliniongoza, kama Spika wangu anaandika barua ya kunisimamisha bila hata ya kuniuliza ananihukumu basi nikate rufaa kwenye Chama changu, ndio sababu yangu ya kuwasiliana na viongozi wangu wa chama kwa maana ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Mwenyekiti wa Wabunge wa CCM ambaye ni Waziri Mkuu.

“Niliwaandikia ujumbe nikiomba ushauri wao na msaada barua hii ilitaka kutumia kunichinja kukata kichwa changu nisiwe Makamu wa Rais na nisiwe Mbunge wa PAP kama angekuwa mtu yeyote angefanya nini?” amehoji Masele.

Aidha, Masele alitumia nafasi hiyo kumuomba radhi, Spika Ndugai, Wabunge kwa yote ambayo yametokea.

“Mheshimiwa Spika nitumie nafasi hii kwa unyenyekevu mkubwa kukuomba radhi wewe binafsi, wewe na familia kwa usumbufu wowote ambao umeupata kupitia sakata hili lakini nitumie nafasi hii kuwaomba radhi wabunge wenzangu kwa usumbufu wowote ambao mmeupata.

“Nitumie nafasi hii pia kuwaomba radhi viongozi wangu wa juu akiwemo rais wangu, Waziri Mkuu ambaye ni Mwenyekiti wetu wa Wabunge wa CCM kwa usumbufu wowote ambao wameupata kutoakana na jambo hili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles