27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Masauni: Uhamiaji imarisheni usalama mipakani

Na Mwandishi maalumu, Loliondo

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusufu Masauni ameitaka Idara ya Uhamiaji nchini kusimamia uingiaji na utokaji wa wageni katika mipaka ya nchi kwa kufuata sheria za nchi.

Waziri Masauni ameyasema hayo leoJumatano Juni 15, 2022 Loliondo, Ngorongoro mkoani Arusha alipofika kukagua maendeleo ya Zoezi la Uwekaji wa Alama za Mipaka katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.

Aidha, Masauni amebainisha kuwa serikali itafanya uhakiki wa kina kubaini uendeshaji wa Asasi za Kiraia nchini kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria na zile zitakazokiuka zitachukuliwa hatua kali za kisheria.

Masauni ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya zoezi na kuwataka wahusika kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakamilika kwa wakati.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mwalimu Raymond Mangwala aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, alimueleza, Masauni kuwa amepokea maelekezo yake na kwamba atahakikisha kuwa hali ya usalama wa wananchi na mali zao inaendelea kuimarishwa wilayani Ngorongoro na kuwa zoezi hilo litaendelea kwa hali ya amani na utulivu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles