27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Masauni: Hatutasita kumchukulia hatua askari asiyefuata maadili

Mwandishi Wetu – zanzibar

SERIKALI imesema haitakuwa tayari kuona Jeshi la Polisi linachafuliwa na baadhi ya askari wasiofuta maadili.
Pia imesisitiza kuwa haitosita kumchukulia hatua askari atakayebanika kukiuka maadili.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, wakati akifunga mafunzo kwa vikundi vya ulinzi shirikishi visiwani hapa ambako jumla ya walinzi 681 walihitimu.


Akizungumza na wahitimu pamoja na askari katika hafla hiyo, Masauni alisema Serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na askari polisi waadilifu huku akiweka wazi kuwapo kwa askari wasio waadilifu.


“Jeshi letu la Polisi lina miiko yake katika utendaji wa kazi zake, lakini wapo askari wachache wanaovujisha taarifa kwa wahalifu, wanasaidia wahalifu kutenda makosa sambamba na kupokea rushwa, hali hiyo haikubaliki na atakayebainika hatutosita kumchukukia hatua kwa mujibu wa taratibu za jeshi,” alisema Masauni.


Naye Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Saleh Mohamed Saleh, aliwataka wananchi kufichua wahalifu wanaowafahamu katika makazi yao ili matendo ya uhalifu yaweze kupungua.


“Polisi Jamii ni dhana pana, tunawategemea wananchi mtusaidie kufichua wahalifu katika maeneo mnayoishi maana uhalifu ukifanyika nyie ndio mnaathirika, hivyo basi ni bora mkawa mabalozi wazuri katika maeneo yenu kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi,” alisema Kamishna Saleh.


Katika mafunzo hayo, jumla ya walinzi shirikishi 681 walihitimu ambao walipitishwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo ukamataji salama, namna ya kuendesha doria, jinsi ya kumfikisha mtuhumiwa kituo cha polisi na elimu jinsi ya kujikinga na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles