30.1 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Masauni asisitiza utoaji elimu barabarani

Mwandishi Wetu -Dar es Salaam

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amesema kuna kila sababu ya kuendelea kutolewa elimu ya usalama barabarani na matumizi sahihi ya barabara ili kupunguza ajali zinazosababisha ulemavu na vifo kwa watu wasio na hatia.

Pia alisema wizara hiyo ipo kwenye mchakato wa kuangalia upya sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuziongezea ukali ili kukabiliana na watumiaji wa vyombo vya moto na hasa waendesha pikipiki ambao wengi wao wamekuwa wakivunja sheria na kusababisha ajali ambazo zinaweza kuepukika.

Masauni aliyasema hayo wakati wa utoaji zawadi kwa wanafunzi na shule za msingi ambazo zimeshinda michoro yenye ujumbe wa usalama barabarani visiwani Zanzibar mwaka huu.

 Shule ya Msingi Mkunazini ilipata Sh milioni 4 kutoka Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, baada ya kuibuka mshindi wa kwanza.

Mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yanayofadhiliwa na Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania ndiyo mara ya kwanza kutolewa visiwani humo.

“Kuna umuhimu mkubwa wa jamii yetu ya Watanzania kwa upande wa Bara na Visiwani kuendelea kupatiwa elimu inayohusu usalama barabarani pamoja na matumizi sahihi ya barabara zetu.

“Nitumie nafasi hii kuipongeza Kampuni ya Puma Tanzania kwa uamuzi wake wa kutoa elimu hii ambapo kwa hapa Zanzibar shule tano za msingi zimepata elimu hiyo na tunaamini itasaidia kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika,” alisema.

Alisema kutolewa elimu ya usalama barabarani kwa wanafunzi kutasaidia kuokoa maisha yao na kuwaepusha na ajali.

“Ajali za barabarani zimeendelea kupungua siku hadi siku, lakini bado kuna changamoto ya baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto na hasa waendesha bodaboda wanavunja sana sheria za barabarani.

“Tumeamua atakeyakamatwa kwa kuvunja sheria za usalama barabarani awekwe mahabusu, kisha apelekwe mahakamani ili sheria ichukue nafasi yake,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Ltd, Dominic Dhanan, alisema  elimu hiyo imetolewa kwa shule tano za msingi za Zanzibar.

“Tumekutana hapa kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wanafunzi wa shule za msingi walioshinda shindano la michoro ya usalama barabarani kwa mwaka 2019 kisiwani Zanzibar,” alisema.

Alisema programu hiyo ilihusisha mafunzo kwa shule za msingi Mwembeshauri, Kisiwandui, Jang’ombe, Nyerere na Mkunazini.

“Wanafunzi wasiopungua 6,500 wamapata elimu hiyo ambayo imekwenda sambamba na uchoraji wa michoro inayohamasisha matumizi sahihi ya barabarani na kufuata sheria zilizopo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles