27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Masauni akabidhiwa majina watuhumiwa dawa za kulevya

MWANDISHI WETU



WANANCHI wa   Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja wamemkabidhi Naibu Waziri  wa  Mambo  ya  Ndani ya Nchi, Hamad  Masauni, orodha ya watu  wanaoshukiwa  kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya visiwani Zanzibar.

Wananchi hao walikabidhi orodha hiyo baada ya Naibu Waziri Masauni kuwataka waorodheshe majina ya watu wanaowafahamu wakituhumiwa kujihusisha na biashara hiyo ambayo imekuwa ikiharibu nguvu kazi ya taifa na kusababisha     matukio ya uhalifu katika sehemu mbalimbali visiwani humo.

Awali,  wakiwasilisha  kero zao kwa nyakati  tofauti, wananchi hao waliiomba serikali  kudhibiti  biashara  hiyo  ya dawa za kulevya  kwa vile   imekua ikishamiri kwa kasi visiwani humo na wanashangazwa na ukimya wa mamlaka husika kuacha biashara hiyo ikizidi kuleta madhara katika jamii.

Akizungumza katika mkutano huo wa hadhara, Masauni aliwaahidi  wananchi  hao  kuchukua  hatua  madhubuti  kukabiliana  na  wauzaji wa dawa za kulevya huku akitoa maelekezo kwa  polisi  kuwakamata watu  wote waliotuhumiwa  na  uchunguzi  uanze  mara moja.

“Hatuwezi  kama  taifa  tukawa  na vijana ambao hawana faida katika jamii.

“Vijana  ni  nguvu kazi ya taifa, tutahakikisha majina yaliyoletwa hapa tunayafanyia  kazi na natoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa na nitahitaji ripoti hiyo ndani ya wiki mbili,” alisema  Masauni.

Akizungumza katika mkutano huo, Kamishna Msaidizi, Saleh Mohamed Saleh, aliwaomba wananchi kuzifikisha  taarifa  za  uhalifu  katika  vituo  vya  Jeshi la Polisi au Serikali ya Mtaa    hatua ziwe zinachukuliwa   kudhibiti  uhalifu  katika  maeneo yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles