27.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Masauni aagiza polisi kutoa dhamana kwa mahabusu kuepuka corona

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amewaagiza makamanda wa polisi na wakuu wa magereza wa mikoa yote nchini, kuwapa dhamana mahabusu wanaokidhi vigezo vya dhamana na kupeleka haraka kesi za watuhumiwa walio gerezani ili kuwaepusha na homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona.

Masauni alisema hayo wakati alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya polisi mkoani Dodoma ambapo alibaini kuwepo msongamano wa mahabusu.

“Maagizo ya Serikali na wataalamu wa afya ni kuepusha misongamano, sasa nimetembelea kituo hiki cha kati nimekuta mahabusu wengine wamekaa siku 14, wengine wanaingia wakiwa wametoka nje huko hali inayosababisha msongamano katika kituo hiki, kuna mahabusu mmoja nimekuta wamemuweka siku tatu hapa na kosa lake ni amekatwa anapita nje ya bunge, hii sio sawa huku hana kosa lolote.

“Sasa natoa maagizo kwa makamanda wa polisi nchi nzima katika kukabiliana na corona wahakikishe mahabusu ambao kesi zao zinadhaminika watolewe, agizo hili pia liende kwa wakuu wa magereza yote nchini kuhakikisha watuhumiwa wote kesi zao zinaharakishwa kupelekwa mahakamani hii ikiwa ni mkakati wa kupambana na corona, sasa watu wamerundikwa tu hakuna kinachoendelea hii si sawa” alisema Masauni.

Pia alizungumza na wananchi waliokusanyika nje ya vituo vya polisi kuwaona ndugu zao huku akisisitiza washughulikiwe haraka kwani wamekusanyana wengi huku Serikali ikiwa imepiga marufuku mikusanyiko.

 “Wananchi wamekuja kuona ndugu zao waliopo mahabusu na kuwaletea chakula tunajua ni haki yao lakini, wahudumie haraka waondoke hii mikusanyiko ishakatazwa ni hatari sana” alisema Masauni.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,554FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles