33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MASAUNI AAGIZA ATAKAYETANGAZA KUNA NJAA AKAMATWE

Na Mwandishi Wetu, Rukwa


Hamad MasauniNAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, ameonya watu wakiwamo wanasiasa wanaoeneza taarifa za uongo za kuwapo baa la njaa, ni kosa na wachukuliwe hatua ikiwamo kukamatwa.

Masauni amesema bado kuna watu wanajichukulia mamlaka ambayo si yao na kueneza uongo kuwa kuna njaa nchini, hilo ni kosa kwa kuwa wanaeneza propaganda ambayo inaweza kusababisha uvunjifu wa amani.

“Hizo ni propaganda za watu wasioitakia mema nchi hii …mtu anapofanya kosa lazima achukuliwe hatua, Jeshi la Polisi liangalieni hili,” alisema.

Masauni alitoa onyo hilo wakati wa ziara yake ya siku moja aliyoifanya jana mkoani Rukwa ambako mkuu wa mkoa huo, Zelothe Steven, alimhakikishia mkoa huo hauna njaa bali una ziada ya kutosha.

“Nyie wenyewe mmemsikia mkuu wa mkoa (Zelothe), amethibitisha hakuna njaa mkoani hapa, lakini si hapa tu, pia mikoa ya Mbeya na Songwe wamenithibitishia hawana njaa.

“Sasa wapo wanasiasa uchwara wanaeneza propaganda kuna njaa, si mamlaka yao kutangaza kuna njaa, kueneza uongo kama huo si sawa kwa kuwa kunaweza kusababisha uvunjifu wa amani nchini, wanastahili kuchukuliwa hatua ikiwamo kukamatwa,” alisema.

Naye Zelothe, alisema hali ya kiusalama katika mkoa huo ni shwari ambapo amani na utulivu umeshamiri kwa kuwa una chakula cha kutosha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles