23.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Masanja asimulia alivyochezea kifinyo

Masanja Mkandamizaji
Masanja Mkandamizaji

Na CHRISTOPHER MSEKENA,

NYOTA wa  vichekesho nchini Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ambaye wiki iliyopita alitawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuvuta jiko, mtoto mrembo Monica, amesema kati ya vitu ambavyo hawezi kuvisahau maishani mwake ni pamoja na adhabu ya kufinywa aliyokuwa akipewa na mama yake.

Akizungumza na Juma3tata, Masanja alisema kuwa nidhamu aliyonayo hivi sasa imetokana na malezi aliyopewa na  marehemu mama yake alipokuwa anamuonya pale alipofanya makosa mbalimbali.

“Utoto una mambo mengi, niseme ukweli kuwa mimi nilikuwa mtundu mno. Lakini mama yangu hakutaka niharibike, alikuwa akiniadhibu kila ninapofanya makosa na mara nyingi alikuwa akinifinya.

“Mama yangu ndiye amenifanya niwe na nidhamu mpaka sasa kwa sababu kipindi kile nakumbuka niliwahi kufinywa hadi  mbele za wageni na kutakiwa kuonyesha tabasamu.

“Nilifinywa kwa makosa tofauti tofauti, si unajua tena tabia za kitoto, fujo za hapa na pale ndiyo vile mama anapitisha mkono chini ya meza na kunifinya halafu ananikazia jicho ili usilie,” anasema Masanja na kuongeza:

“Lakini mimi najivunia kwa hilo, wala simlaumu mama yangu, maana alininyoosha na kunitengenezea maisha ya nidhamu hadi utu uzima huu unaoniona nikiwa tayari nimeshaingia kwenye ndoa yangu. Nidhamu niliyonayo, sifa ziende kwa mama yangu.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles